POLISI ARUSHA YASHTUKIA “DILI”


US1
Askari wa Jeshi la Polisi wa wilaya ya Arusha na vikosi vingine wakiwa wanamsikiliza Afisa Masoko wa URA SACCOS toka makao makuu  Mkaguzi wa Polisi Shabani Jumbe alipokuwa anatoa elimu hiyo katika ukumbi wa bwalo la Polisi uliopo jijini hapa. (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)
US2
Mmoja wa wanachama cha Ura saccos CPL Ezekiel akiuliza swali lililokuwa linamtatiza kwa muda mferu ambalo baadae lilijibiwa vizuri na Afisa Masoko huyo toka makao makuu (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)
US3
Mkuu wa kituo kikuu cha Polisi Arusha Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Thomas Mareko akitoa ufafanuzi kwa askari waliohudhuria kikao hicho juu ya Ura Saccos kulia kwake ni Mkaguzi wa Polisi shabani Jumbe ambaye pia ni Afisa Masoko wa chama hicho. (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)
US4
Baadhi ya askari wakiwa wanajaza fomu za Ura Saccos kwa ajili ya kujiunga na chama hicho mara baada ya kupata elimu iliyoeleweka toka kwa Afisa Masoko toka Makao makuu Mkaguzi wa Polisi Shabani Jumbe. (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)
 ………………………………………………………………………………………………………………
Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha
Ikiwa tunauaga mwaka 2015 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2016 masaa machache yajao baadhi ya askari wa Jeshi la Polisi Mkoani hapa wanaonekana kufurahia baada ya wengi wao kupata elimu ya Chama cha Ushirika cha Akiba na Mikopo Ura Saccos iliyokuwa inatolewa na Afisa Masoko na uelimishaji wa Chama hicho toka Makao Makuu Mkaguzi wa Polisi Shabani Jumbe.
Elimu hiyo iliyotolewa na Afisa Masoko huyo, iliwafanya askari zaidi ya 100 wabadilishe mawazo ya kujitoa kwenye Chama hicho na badala yake walichukua fomu za kujiunga na Chama hicho kwa ambao hawakuwa wanachama na kwa wale ambao walikuwa wanachama waliamua kuongeza kiwango cha makato kwa asilimia 50 hadi 90 huku wengine wakiendelea kupiga simu kwa msimamizi wa Ura Saccos mkoa wa Arusha PC Said wakitaka fomu za kujiunga na Chama hicho.
Awali akitoa elimu hiyo katika wilaya za Arumeru, Monduli, Longido na Arusha mjini, Afisa Masoko huyo  alisema tatizo kubwa lililokuwepo ni ufinyu wa elimu kwa wanachama na wasio wanachama na kufafanua kwamba wameamua kutoka ofisini na kuwafuata mikoani kwa lengo la kuwaelimisha ili waone umuhimu wake.
Alisema wanachama wengi walikuwa hawajui sababu zinazosababisha kupata mikopo midogo ndani ya Chama hicho kwamba zinatokana na kiasi cha Akiba wanazoweka kwa mwaka kuwa ni kidogo huku akisema wengi wao wanaweka elfu kumi kwa mwezi.
“Sasa mfano utakuta mwanachama anaweka Tsh. 10,000/= Kwa mwezi ndani ya mwaka mmoja anajikuta ana Tsh 120,000/= alafu baada ya miaka mitatu anaomba mkopo hivi unafikiri utapata kiasi gani”? Alihoji Afisa Masoko huyo Shabani Jumbe ambaye pia ni Mkaguzi wa Polisi.
Alisema Chama hicho kwa sasa kimeweka utaratibu wa kumwekea Mwanachama 3% kwa kila laki tano ambayo atakuwa ameweka akiba ndani ya chama hicho ambayo inaitwa riba juu ya Akiba.
Akitoa ufafanuzi juu ya utaratibu wa Mwanachama kutoa Akiba yake ndani ya siku 90 na si chini ya hapo alisema hii inatokana na idadi ya wanachama wanaochukua mikopo kuwa kubwa lakini pia inatoa fursa ya kukusanya madeni toka kwa wanachama wengine waliokopa.
“Wanachama wengi wanashindwa kutofautisha kati ya Akiba na Amana ambapo kwenye Amana mwanachama anaweza kutoa fedha yake wakati wowote na haina notisi ya siku 90 lakini kwenye Akiba utaratibu wetu ni siku 90 lakini pia karibu askari 21,000 kwa mwezi wanachangia Tsh 10,000 hali ambayo inakwamisha uwezo wa chama kukua na kusababisha kushindwa kutoa mikopo mikubwa kwa wanachama”. Alisema Afisa Masoko huyo.
Alisema mbali na kuweka akiba kwenye chama hicho lakini pia wanachama wanatakiwa wawe wananunua hisa zaidi ya zile za msingi ambazo ni 20 lakini tu zisizidi 20% ya hisa zote za chama hicho ili kuondokana na hali ya uchangiaji tu bali pia wawe wamiliki wa sehemu ya chama na mwisho wa mwaka kupata gawio.
Alisema uwepo wa Chama hicho ambacho kwa sasa kina wanachama wanaokadiriwa 34,000 kimesaidia kuweka usimamizi wa nidhamu ya fedha Kwani ni watu wachache wenye uthubutu wa kuwa na utamaduni wa kuweka Akiba kila mwezi na kuongeza kwamba mpaka sasa toka mwaka 2007 kimetoa mikopo kwa wanachama wake kiasi cha Tsh. 82.3 bilioni.
Naye Mkuu wa kituo kikuu cha Polisi cha Arusha Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Thomas Mareko ambaye kitaaluma ni Mhasibu aliwataka askari kuongeza viwango vya akiba zao hali ambayo itawasaidia kupata mikopo mikubwa na pia kunufaika na riba ya aslimia tatu ya kila mwezi kwa watakaoweka kuanzia Tsh. 500,000/=.
Alisema awali askari walikuwa na wasiwasi juu ya Chama hicho lakini baada ya elimu walielewa hivyo aliwataka wachangamkie fursa hiyo ya kupata mikopo yenye riba nafuu.
Kwa upande wao baadhi ya askari waliopata elimu hiyo kutoka wilaya mbalimbali za Mkoa huu walisema wameweza kubadilishwa mawazo yao ya kutaka kujitoa kwenye chama hicho na hivyo wameamua kuongeza akiba hali ambayo itasaidia kuinua uchumi wao siku za usoni.
“Nashukuru sana kwa Inpekta Shabani Jumbe kutoa elimu hii binafsi nimeifurahia na kuongeza ufahamu kwa upande wangu hali iliyonipa hamasa ya kuchukua fomu na kuongeza akiba yangu toka 10% hadi 50% kwa mwezi”. Alisema Asia Matauka ambaye ni Mkaguzi wa Polisi na kushauri kwamba wajenge matawi katika mikoa yote.
“Baada ya kupata elimu nimegundua kwamba Chama hiki cha ushirika ni chama muhimu sana kwa askari na mimi nimeamua kuongeza akiba yangu toka elfu 10 hadi elfu 80 kwa mwezi” .Alisema D/C Anzelim toka wilaya ya longido.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI