HOSPITALI YAKABILIWA NA UHABA WA VYUMBA VYA KUHUDUMIA WAGONJWA


Mkuu wa Mkoa wa Arusha Daudi Felix Ntibenda akizungumza na Wagonjwa katika Hospitali ya Ngarenaro iliyoko jijini Arusha ,hospitali hiyo inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa vyumba vya kuhudumia wagonjwa pamoja na gari la wagonjwa
Na Woinde Shizza,Arusha.
Hospitali ya Ngarenaro inakabiliwa na uhaba wa vyumba vya kuhudumia wagonjwa pamoja na kukosekana kwa miundombinu imara ya maji katika chumba cha upasuaji hivyo kuhitaji upanuzi pamoja na ukarabati wa hospitali hiyo ambayo inahudumia zaidi ya Wakazi 74000 wa kata ya Ngarenaro jijini Arusha.
Akizungumzia changamoto hizo Daktari Mfawidhi wa Hospitali hiyo Josephat Kivuyo katika taarifa yake kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha ,Kivuyo amesema kuwa hospitali hiyo inahitaji upanuzi na ukarabati ili kuweza kuboresha huduma za afya ambazo zinahitajika na wananchi wengi.

Daktari huyo Mfawidhi alisema kuwa changamoto nyingine ni uhaba wa magari ya wagonjwa maarufu kama Ambulance kwani gari lililopo ni la zamani na haliwezi kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa kama inavyotarajiwa.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Daudi Felix Ntibenda amewataka wananchi na wadau mbalimbali kuunganisha nguvu katika kuboresha huduma kwa kufanya ukarabati ambao tayari umeshaanza ili kuboresha mazingira bora kwa wananchi na wahudumu wa afya.

Pia Amewataka Wahudumu wa Afya kuepuka kutoa lugha mbaya kwa wagonjwa na kuwahudumia vizuri ili kupunguza malalamiko katika sekta ya afya ambayo inahudumia watanzania wengi.Alisema Ukarabati wa Kituo cha Afya cha Ngarenaro unaendelea na tayari hivyo nguvu ya serikali n wadau wa maendeleo inahitajika katika kuhakikisha kuwa vituo hivi vinakuwa katika mazingira rafiki ya utoaji huduma za afya.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.