KONGAMANO LA UWEKEZAJI KATI YA WATANZANIA NA WARUSI 28 APRILI 2016, JNICC, DAR ES SALAAM


RUSSIA1RUSSIA2
Tunayo furaha kubwa kuwakaribisha kwenye Kongamano la Uwekezaji kati ya Watanzania na Warusi litakalofanyika siku ya Ijumaa tarehe 28 Aprili 2016 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Kongamano hili limeandaliwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kikishirikiana na Russian Export Club, Mfuko wa Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Ubalozi wa Tanzania nchini Urusi na Ubalozi wa Urusi nchini Tanzania; kwa usimamizi wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji nchini Tanzania, Wizara ya Biashara na Viwanda ya Urusi na Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kongamano la Uwekezaji kati ya Tanzania na Urusi 2016 linatarajia kuwaleta pamoja kundi la wawakilishi wa Serikali ya Urusi, wenye viwanda na wafanyabiashara wakubwa kwa lengo kushirikiana na kuimarisha mazingira ya biashara na uwekezaji baina ya nchi hizi mbili. Kupitia mahusiano haya ya ushirikiano wa kiuchumi baina ya Tanzania na Urusi kutaongeza zaidi ushiriki wa makampuni ya Kirusi katika kufanya biashara na uwekezaji hapa nchini.
Ujumbe wa wafanyabiashara wa Kirusi unatarajiwa kufikia watu 60 ukiongozwa na Mheshimiwa Denis  Manturov, Waziri wa Biashara na Viwanda wa Serikali ya Shirikisho ya Urusi. Ujumbe huu pia utajumuisha viongozi wengine wa serikali, Wakuu wa makampuni na wawakilishi wa vyombo vya habari kutoka Urusi. Kongamano hili litajikita zaidi katika ushirikiano wa kiuchumi katika sekta za nishati, usafirishaji, miundombinu, mafuta & gesi, madini, huduma za fedha, kilimo na viwanda.
Wakati wa Kongamano hili, yatafanyika majadiliano ya moja kwa moja na mikutano ya Biashara-kwa-Bisahara (B2B), mikutano ya Serikali na Wafanyabiashara (B2G) na Serikali na Serikali (G2G). Wafanyabiashara  wa kutoka Urusi watapata pia fursa ya kutembelea maeneo ya viwanda ya EPZA ili kujionea uzoefu wa moja kwa moja kuhusu sekta ya viwanda hapa nchini.
Ushirikiano baina ya Tanzania na Urusi katika nyanja za Uwekezaji na Biashara unaonesha kuwa mzuri kwa miaka ya hivi karibuni ingawa bado ni mdogo ukilinganisha na fursa zilizopo. Hivyo basi, kwa kupitia Kongamano hili, tutatoa nafasi  ya kufungua na kujionea fursa lukuki zilizopo za kiuwekezaji na kibiashara baina ya nchi hizi mbili, pamoja na kukuza utalii.
Tunawakaribisha sana Wafanyabisahara wa Tanzania!
Imetolewa na: Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC)
Tarehe: 26 Aprili 2016

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.