MKURUGENZI WA HALMASHAURI WA MJI KAHAMA APEWA SIKU TISINI NA WAZIRI WA AFYA UMMY MWALIMU AWE AMENUNUA MASHINE YA MIONZI X RAY.


1Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto akiongea na baadhi ya wakazi wa kahama waliofika hospitalini hapo kuangalia wagonjwa wao.
2Waziri.Ummy Mwalimu akitoa angalizo kwa wagonjwa waliofika kupata matibabu kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa wa.shinyanga
3Mh.Ummy Mwalimu akiwaelekeza kamati ya afya ya wilaya ya kahama mahali linapotakiwa kuwekwa bango linaonesha huduma za wazee inapopatikana.
4Mkuu wa wilaya ya Kahama Mh.Vita Kawawa(Katikati) akionesha kwa vitendo bango hilo linapotakiwa kuwekwa,kushoto ni Mh.Ummy Mwalimu na kulia ni mkurugenzi wa halmashauri ya mji kahama Anderson Msumba.
5Mfamasia Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Luciano Lodrick akimpatia maelezo waziri ,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto jinsi ya utengenezaji wa maji tiba.
6Waziri Ummy Mwalimu akiangalia kifaa cha kutengenezea maji tiba kwenye.hospitali ya.rufaa ya mkoa wa shinyanga.
7Mh.Ummy Mwalimu akiangalia matangazo yaliyobandikwa kwenye ubao hospitanini hapo.Waziri Ummy ameuagiza uongozi wa hospitali hiyo kubandika gharama za matibabu pamoja na namba za simu kwa ajili ya kupokelea maoni na malalamiko toka kwa wananchi.
………………………………………………………………………….
Na.Catherine Sungura,kahama
Mkurugenzi wa halmashauri wa mji kahama amepewa siku tisini awe amenunua mashine ya mionzi (x ray)kwa ajili ya hospitali ya mji kahama
Agizo hilo amepewa jana na Waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Ummy mwalimu wakati alipotembelea hospitali hiyo pamoja na kuongea na watumishi wa kada ya afya wa wmji huo.
Waziri Ummy alisema ametoa agizo hili ili kuweza kurahisisha usumbufu wanaupata wananchi wa wilaya hiyo kwa kwenda kupata huduma nje ya hospitali ambapo wakati mwingine vipimo hivyo vinakuwa havisomeki vizuri kwa kukosa viwango vinavyostahili za mashine hizo.
Hata hivyo waziri ummy alisema upatikanaji wa mashine hizo itapunguza malalamiko mengi toka kwa wananchi kwa ukosefu wa kifaa tiba hicho ili kwani hospitali hiyo hivi sasa inahudumia wananchi zaidi ya milioni moja hususan toka wilaya zote za wilaya hii
Aidha, alizitaka halmashauri zote mjini kuweza kuwekeza kwenye huduma za vifaa tiba ambavyo inarahisisha kugundua matatizo yanayowakabili wananchi wanaofika kwenye kupata huduma na hivyo kuwapatia matibabu stahili wagonjwa wanaofika kupata matibabu kwenye vituo vya kutolea huduma nchini.
?siku hizi lazima muwekeze kwenye kununua vifaa tiba ili kuweza kupata kutoa huduma nzuri ,pesa mnakusanya na kahama ni halmashauri tajiri,mkurugenzi nakupa siku tisini uwe umenunua mashine hiyo
Naye mkuu wa Wilaya hiyo Mh. Vita kawawa amemuahidi waziri huyo kwamba amepokea maagizo yote aliyoyatoa na atayafuatilia ili kuweza kutatua malalamiko ya wananchi na yale ya watumishi wa kada ya afya

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.