MWALIMU: KIPINDUPINDU HAKIENEZWI KWA KUROGWA


indexnn
Na.catherine Sungura,Kyela 
Wananchi wa wilaya ya kyela wametakiwa kuachana na mila potofu na kupelekea kufanya mauaji ya watu kwa kuhusisha ugonjwa wa kipindupindu ni ugonjwa unaoletwa kwa imani ya kishirikina
Hayo yamesemwa leo na waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto  Ummy Mwalimu,wakati alipofanya ziara katika wilaya hii na kuongea na watendaji wa halmashauri.
Mh.Ummy alisema ameshangazwa na baadhi ya wananchi katika kijiji cha unyakyusa kujichukulia sheria mkononi na kuwauwa wanawake watatu kwa madai ndio wanaoneza ugonjwa huo.
Naye mkuu wa wilaya ya kyela dkt. Thea Ntara alisema kamati yake ya ulinzi na usalama imeshawakamata watuhumiwa wawili wa tukio hilo na kuwafikisha mahakamani ingawa bado mtuhumiwa mmoja aliyekimbilia nchi jirani ya malawi anatafutwa.
Matukio hayo yametokea mwezi februari na machi mwaka huu.
Wilaya ya kyela ilipokea mgonjwa wa kipindupindu novemba 2015 na hadi kufikia machi 2016 jumla ya wagonjwa 405 waliugua ambapo vifo vilikua 8. Kwa sasa wilaya hii haina mgonjwa wa kipindupindu
Hali ya kipindupindu nchini imekua ni tatizo kubwa nchini,takribani mikoa yote tanzania bara imekubwa na ugonjwa huu tangu ulipotiwe mwezi agosti mwaka jana,isipokuwa kwa mkoa wa Ruvuma na Njombe ambapo hawajaripoti mgonjwa wowote hadi Sasa
Ripoti ya wizara ya afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto ya tarehe 4 machi mwaka huu inaonesha jumla ya wagonjwa 20,294 wametolewa taarifa na kati ya hao 320 wamepoteza maisha.
Kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka,mwenendo wa kipindupindu unaashiria idadi ya wagonjwa nchini inaongezeka

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.