SERIKALI INAENDELEA KUFANYA KAZI KWA USHIRIKIANO NA WANAHABARI NCHINI.

E1
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye akichangia Hotuba ya Ofisi ya Waziri Mkuu 25/04/2016 jioni bungeni mjini Dodoma na kusisitiza kuwa Serikali inaendelea kufanya kazi kwa ushirikiano na wanahabari nchini
E3
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango (aliyesimama) akichangia Hotuba ya Ofisi ya Waziri Mkuu 25/04/2016 jioni bungeni mjini Dodoma  na kusisitiza Wizara yake inavyochangia masuala mbalimbali ya kiuchumi na kijamii nchini.
E4
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Dkt. Possy Abdallah akichangia Hotuba ya Ofisi ya Waziri Mkuu 25/04/2016 jioni bungeni mjini Dodoma na kusisitiza juu ya Serikali inavyosimamia suala la watu wenye ulemavu nchini. Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira Walemavu Jenista Muhagama na kulia ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Anthony Mavunde.
E5
Wabunge wakifuatilia mjadala wa Hotuba ya Ofisi ya Waziri Mkuu 25/04/2016 jioni bungeni mjini Dodoma.
(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO)
…………………………………………………………………………………………………
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
Serikali inaendelea kufanya kazi kwa ushirikiano na wanahabari nchini ili kuhakikisha wananchi wanapata taarifa mbalimbali zinazofanywa na Serikali yao katika nyanja za kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni ili kuhakikisha Watanzania wanafikia maendeleo yao na taifa kwa ujumla.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye alipokuwa akichangia Hotuba ya Ofisi ya Waziri Mkuu 25/04/2016 jioni bungeni mjini Dodoma.
“Waandishi wa habari wapo huru kuuliza maswali kwa Wabunge na kuandika habari kupitia vyombo vyao na kuwapatia wananchi taarifa mbalimbali zinazoendelea bungeni” alisema Waziri Nape.
Kuhusu idadi ya vyombo vya habari nchini, Waziri Nape amesema kuwa Tanzania ni nchi yenye vyombo vingi vya habari yakiwemo magazeti, redio na televisheni ambavyo ni ishara wazi kuwa vyombo hivyo vipo huru kufanya kazi zao kwa kuzingatia maadili ya taaluma ya tasnia ya habari pamoja na katiba, Sheria, kanuni na taratibu za nchi.
Waziri huyo alisema kuwa Tanzania sio nchi ya kwanza kutokurusha matangazo ya bunge moja kwa moja (live), utaratibu huo unafuatwa na Mabunge yote ya jumuiya ya Madola.
Waziri Nape amesema kuwa bado Serikali inakusudia kuboresha mazingira ya waandishi wa habari ili waweze kufanya kazi zao kwa hali ya uhuru hasa wanapotimiza majukumu yao ya kiundishi wa habari.
Aidha, amewashukuru wabunge kwa uzalendo wao wa kubaki ndani ya bunge na kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo ya nchi yao kwa manufaa ya wananchi wanaowawakilisha.
Kwa upande wake Mwanasheria Mkuu wa Serikali Gorge Masaju amewashukuru wabunge kutimiza haki yao ya Kikatiba kuingia Bungeni na kushiriki mijadala mbalimbali kulingana na ratiba iliyopo
Kwa mujibu wa ibara ya 63 (2), Bunge itakuwa ndicho chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano ambacho kitakuwa na madaraka, kwa niaba ya wananchi, kuisimamia na kuishauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake.
Kuhusu matangazo ya Bunge kurushwa moja kwa moja, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Masaju alisema kuwa Watanzania wanaendelea kupata taarifa kupitia vyombo mbalimbali vya habari nchini.
Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara 18. (2) Kila raia anayo haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio mbalimbali nchini na duniani kote ambayo ni muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi, na pia juu ya masuala muhimu kwa jamii.
Akitoa ufafanuzi wa ibara hiyo Masaju alisema kuwa haki ya kupewa taarifa, siyo haki ya kuonekana na vile vile maamuzi ya Bunge hayafanywi kwa muonekano, bali hufanywa kwa majadiliano ya Wabunge wakiwa Bungeni.
Bunge litaendelea na vikao vyake Jumatano Aprili 27, baada ya kuahirishwa kwa mapumziko ya maadhimisho ya Sherehe za miaka 52 ya Muungano wa Tanzania na ambapo mwaka huu Watanzania wametakiwa kuiadhimisha wakiwa majumbani au wakiwa katika shughuli zao binafsi.
Mapema mwezi huu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alielekeza fedha zilizopangwa kutumika katika maadhimisho hayo ambazo ni sawa na Shilingi bilioni 2 za Tanzania zitumike kupanua barabara ya Mwanza Airport katika eneo linaloanzia Ghana Quarters hadi uwanja wa ndege wa Mwanza ili kupunguza adha ya msongamono wa magari katika barabara hiyo Jijini humo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.