WABUNGE WA AFRIKAMASHARIKI WATEMBELEA THE GUARDIAN

 NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said
……………………………………………………..
Wabunge wa bunge la Arika Mashariki, (EALA), kutokaTanzania, wameendelea na ziara yao ya kutembelea vyombovya habari hapa nchini, ikiwa ni mkakati wa Jumuiya hiyo, kushirikisha vyombo vya habari ili kuwafahamishawananchi wa nchi hizo manufaa ya jumuiya hiyo kwao. LeoAprili 13, 2016, wabunge hao wakiongiozwa na Mwenyekiti wao Mh. Makongoro Nyerere, wametembelea kampuni ya The Guardian, wachapishaji wa magazeti ya The Guardian, Nipashe na Lete Raha, na kupata fursa ya kuelezwa shughuli zifanywazo na waandishi wa habarikwenye kampuni hiyo ambapo walitembelea kitengo cha habari mtandao, (E-NEWS), kitengo cha usanifu gazeti na kumalizia kwa mkutano wa kubadilishana mawazobaina ya wabunge hao na uongozi wa chumba cha habari cha The Guardian. Pichani, msanifu wa gazeti la The Guardian, Ben Mgana (aliyekaa), akiwaonyesha jinsi gazeti hilo linavyoandaliwa kabla ya kuchapishwa. Wakwanza kushoto ni Mhari Mtendaji wa gazeti hilo, Wallace Maugo, Mkuu wa chumba cha Habari cha The Guardian, Jesse Kwayu, (wapili kushoto) na wabunge wa hilo wakiongozwa na wmenyekiti wao Mh. Makongoro Nyerere (watatu kulia)
 MhaririMtendaji wa The Guardian, Wallace Mauggo, (watatu kushoto) na Mhariri Mkuu wa Chumba cha Habari cha The Guardian Limited, Bw. Jesse Kwayu) wakiwaonyesha wabunge hao baadhi ya magazeti yanayochapishwa na kampuni hiyo
 Mwenyekiti wa wabunge wa EALA-Tanzania, Mh. Makongoro Nyerere, 9wapili kulia), akisalimianana Mkuu wa kitengo cha habari mtandao (E-NEWS), cha The Guardian Limited, Mashaka Mgeta, wakati wabunge hao walipotembelea chumba cha Habari cha The Guardian Mikocheni jijini Dar es Salaam

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

𝙂𝘼𝙈𝙊𝙉𝘿𝙄 𝙆𝘼𝘾𝙃𝙀𝙕𝘼 𝙆𝙄𝘽𝙄𝙉𝙂𝙒𝘼.