SERIKALI YASHIRIKISHA VIJANA KUJADILI AFYA YA UZAZI NA VVU/UKIMWI


tac1Mkurugenzi Mtendaji Tume ya Kudhibiti Ukimwi Bibi. Fatma Mrisho akifungua mkutano wa mwaka wa wadau wa masuala ya vijana kujadili masuala mbalimbali ya vijana leo Jijini Dar es Salaam
tac3Baadhi ya vijana na wadau wa vijana akifuatilia kwa makini mada zilizokua zikiendelea wakati wa mkutano wa mwaka wa wadau wa masuala ya vijana kujadili masuala mbalimbali ya vijana leo Jijini Dar es Salaam
tac2Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Dkt. Abdallah Possi akizungumza na vijana na wadau wa vijana (hawapo pichani) wakati wa mkutano wa mwaka wa wadau wa masuala ya vijana kujadili masuala mbalimbali ya vijana leo Jijini Dar es Salaam.
tac4Mkurugenzi Mtendaji Tume ya Kudhibiti Ukimwi Bibi. Fatma Mrisho (kushoto) akiteta jambo na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Dkt. Abdallah Possi wakati wa mkutano wa mwaka wa wadau wa masuala ya vijana kujadili masuala mbalimbali ya vijana leo Jijini Dar es Salaam
tac5Vijana wanaoishi kwa matumaini wakitoa nasaha kwa vijana wengine jinsi ya kujitunza na kufikia malengo waliyojiwekea wakati wa mkutano wa mwaka wa wadau wa masuala ya vijana kujadili masuala mbalimbali ya vijana leo Jijini Dar es Salaam
tac6Balozi wa Kilimanjaro marathoni changia dola elfu tano kuondoa unyanyapaa, maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi na vifo vitokanavyo na ukimwi Bw. Mrisho Mpoto akiteta jambo na vijana jinsi ya kupambana na VVU leo jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa mwaka wa wadau wa masuala ya vijana kujadili masuala mbalimbali ya vijana.
tac7Kikundi cha ngoma kikitumbuiza wakati wa mkutano wa mwaka wa wadau wa masuala ya vijana kujadili masuala mbalimbali ya vijana leo Jijini Dar es Salaam
tac8Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Dkt. Abdallah Possi (katikati waliokaa) katika picha ya pamoja na viongozi na vijana walioshiriki katika mkutano wa mwaka wa wadau wa masuala ya vijana kujadili masuala mbalimbali ya vijana leo jijini Dar es Salaam. Wanne kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji Tume ya Kudhibiti Ukimwi Bibi. Fatma Mrisho
Picha na: Genofeva Matemu  – Maelezo.
……………………………………………………………………………………………….
Na: Genofeva Matemu – Maelezo
Serikali imedhamiria kuhakikisha kuwa vijana wote nchini wanashirikishwa kikamilifu na kupatiwa huduma zinazotakiwa ili kumaliza uwepo wa maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi, kupunguza ubaguzi na unyanyapaa unaotokana na ukimwi pamoja na kupunguza vifo vitokanavyo na ukimwi kwa vijana.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Dkt. Abdallah Possi alipokua akifungua mkutano wa mwaka wa wadau wa masuala ya vijana leo Jijini Dar es Salaam.
Dkt. Possi amesema kuwa asilimia 2 ya maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi yapo miongoni mwa vijana wenye umri kati ya miaka 15 hadi 24 ambapo ushamiri kwa vijana wa kike uko juu zaidi ya ule wa vijana wa kiume hasa katika umri wa miaka 23 hadi 24.
Akizungumza wakati wa mkutano huo Mkurugenzi Mtendaji Tume ya kudhibiti Ukimwi Bibi. Fatma Mrisho amesema kuwa Tume inaendelea kushirikiana na jamii kuhakikisha kuwa watoto na vijana wanapata kinga na huduma stahiki kupunguza utegemezi hivyo kuwafanya vijana kujiamini na kujitokeza kupambana na VVU/UKIMWI
“Vijana ni nguvu kazi ya taifa la leo, wakipatiwa nafasi ya kujitambua na kuwasilisha hisia zao utegemezi ndani yao utapungua, ni vyema vijana wakaandaliwa mazingira ambayo watakua huru kushiriki katika masuala ya VVU na UKIMWI” Alisema Bibi. Mrisho.
Aidha Bibi. Mshiro amemtaka kila kijana aliyeshiriki mkutano huo kubeba mambo muhimu manne na kuwafikishia vijana wengine kumi waliopo vijiweni, maofisini ama sehemu nyingine yeyote ile ili kuweza kusambaza elimu waliyoipata kwa kila kijana nchi nzima na kuokoa afya za vijana wenzao.
Kwa upande wake kijana anayeishi kwa matumaini Bi. Wittiness Nakanje ameiomba serikali kuanzisha kliniki maalumu za vijana wanaoishi na VVU/UKIMWI ili kuwaweka vijana kuwa huru kujitokeza kwa wingi kupima afya zao na kupata elimu ya VVU na UKIMWI.
Kulingana na utafiti wa viashiria vya UKIMWI kwa mwaka 2011/2012 tanzania inajumla ya vijana milioni 12 wa umri wa 10 hadi 19 ikiwa ni asilimia 24 na milioni 16 wa umri wa miaka 19 hadi 24 ikiwa ni asilimia 24 ya Watanzania wapatao milioni 44, idadi hiyo ya vijana inajumuisha wasichana wapatao 7,430,840 na wavulana 6,924,612.
Kwa mujibu wa Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 vijana wa umri wa miaka 19 hadi 24 wako 3, 954,039  ambapo wasichana idadi yao ni 2,160,986 sawa na asilimia 55 na wavulana 1,793,053 sawa na asilimia 45.
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

ANGALIA PICHA NDEGE KUBWA YA ABIRIA DUNIANI ILIYOANZA SAFARI NDEFU ZAIDI!

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

LICHA YA UZURI WAKE MWANADADA ELIZABETH MICHAEL a.k.a LULU SI MALI KITU MBELE YA RAY, AMKWEPA KUOGOPA AIBU.

IJUE HISTORIA YA UHASIMU WA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI

NCHI YA URUSI NDIYO NCHI INAYOONGOZA KWA KUWA NA UBORA WA ELIMU NA VYUO DUNIANI.

YANGA SC WAANZA KAZI AFRIKA LEO…WANAKIPIGA NA U.S.M. ALGER SAA 4:00 USIKU ALGERIA

DC MJEMA AONJA ADHA YA MAFURIKO AKIKAGUA ATHARI ZA MAFURIKO ILALA

KWA HERI KAMANDA WETU ABBAS KANDORO