SERIKALI YATAIFISHA SHAMBA LA LOWASSA MONDULIWaziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akitoa tamko bungeni, Dodoma jioni hii, kwamba shamba la Makuyuni ililopo wilayani Monduli, Arusha, linachomilikiwa na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, serikali linachukuliwa na kuligawa kwa wananchi wa wilaya hiyo. Habari, Picha na Richard Mwaikenda;Kamanda wa Matukio Blog

Ombi la kutaka shamba hilo lichukuliwe lilitolewa na Mbunge wa Jimbo la Monduli,  Julius Karanga (Chadema), wakati akichangia majadiliano ya makadirio ya Bajeti ya wizara hiyo, bungeni Dodoma  leo.

Waziri Lukuvi, amejibu kuwa serikali imesikia kilio chako na cha wananchi wa Monduli  kuhusu shamba hilo na kwamba sasa shamba hilo ambalo wakati wa Rais Benjamin Mkapa lilitaifishwa kutoka kwa Mfanyabiashara Stein na kuamuru ligawiwe kwa wananchi lakini lilichukuliwa na Lowassa.

Amesema kama Mheshimiwa Mbunge, Karanga alikuwa hajui kwamba shamba hilo la makuyuni alijimilikisha Lowassa, basi imekula kwake,  shamba linachukuliwa na serikali na kuligawa kwa wananchi. Najua kazi ni ngumu kwako, lakini naomba tushirikiane shamba hili liende kwa wananchi.

"Ninayo hati hapa ya shamba hilo  imesainiwa na Lowassa, nasema tutairekebisha ili shamba hilo ligawiwe kwa wananchi." alisema Lukuvi huku wabunge wengine wakicheka.

Alisema kuwa wakati shamba hilo anajilimikisha. Lowassa alikuwa waziri wa nchi ofisi ya Ofisi ya Waziri Mkuu.
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

DC MJEMA AONJA ADHA YA MAFURIKO AKIKAGUA ATHARI ZA MAFURIKO ILALA

ZAKIA MEGHJI AWATIA HAMASA GIRL GUIDES, ATAKA WAWE JASIRI

DC MKURANGA AZINDUA MRADI WA MASHAMBA MJI YA NAMAINGO MSOLWA

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

IJUE HISTORIA YA UHASIMU WA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI

TGGA WAMUAGA BOSS WA GIRL GUIDES AFRIKA KWA HAFLA KABAMBE

ANGALIA PICHA NDEGE KUBWA YA ABIRIA DUNIANI ILIYOANZA SAFARI NDEFU ZAIDI!

Wasafi TV kuanza kurusha matangazo yake leo (+video)