SHERIA MPYA YA USHIRIKA YAWANUFAISHA WAKULIMA WA TUMBAKU



Na Fatma Salum- MAELEZO, Dodoma.

Serikali imebainisha kuwa Sheria Mpya ya Ushirika (Sheria namba 6 ya mwaka 2013) imesaidia kupunguza changamoto za wanachama wa Vyama vya Ushirika pamoja na wakulima wa Tumbaku nchini.

Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mhe. Tate William Ole-Nasha aliyasema hayo leo bungeni Mjini Dodoma wakati akijibu maswali ya wabunge kwenye kipindi cha maswali na majibu.

Mhe. Ole-Nasha alisema kuwa baadhi ya marekebisho ya Sheria hiyo yanayowanufaisha wanachama wa Vyama vya Ushirika wakiwemo wakulima wa tumbaku ni pamoja na kuwachukulia hatua viongozi wabadhirifu wa vyama hivyo.

“ Katika maeneo yanayolima tumbaku viongozi wabadhirifu wa Vyama vya Ushirika 26 Mkoani Ruvuma wakiwemo Maafisa Ushirika wawili wamesimamishwa kazi na kufikishwa mahakamani.” alisema Ole-Nasha.

Pia Mhe. Ole-Nasha alifafanua kuwa sheria ya sasa inakataza vyama kukopa zaidi ya asilimia 30 ya mali zake (Own Capital) ili kuzuia vyama hivyo kuingia kwenye madeni makubwa yasiyolipika na hatimaye kusababisha migogoro ndani ya vyama.

Akizungumzia mafanikio upande wa tozo, Ole-Nasha lisema kuwa kuanzia sasa Mkutano Mkuu utakuwa chini ya uenyekiti huru utakaochaguliwa na wajumbe wa mkutano huo kinyume na awali ambapo Mwenyekiti wa Bodi ya Tumbaku ndiye aliyekuwa Mwenyekiti wa Mkutano Mkuu. 
 “Lengo ni kulinda maslahi ya wakulima ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa tozo zote zinazoidhinishwa na Mkutano Mkuu zinakuwa na maslahi kwa wakulima wa Tumbaku.” Aliongeza Ole-Nasha.

Kwa mujibu wa Ole-Nasha Serikali inatambua uwepo wa kodi nyingi na tozo kwenye mazao mbalimbali ya chakula na biashara hivyo kwa kushirikiana na wadau imedhamiria kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara katika sekta ya kilimo kwa kupitia upya taratibu, vibali, tozo, kodi, ushuru na ada nyingine zinazotozwa ili kutoa nafuu kwa wakulima.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI