TRA KUGAWA EFD’S 5700 KWA WAFANYABIASHARA


TRA1Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Alphayo Kidata  akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusu mwenendo wa makusanyo ya mapato nchini kulia ni Kamishna wa kodi za ndani Bw. Yusufu Salum.
(Picha na Raymond Mushumbusi MAELEZO)

Na Lilian Lundo MAELEZO
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imejipanga kugawa jumla ya mashine 5700 za (Electronic Fiscal Devices) EFD’s kwa wafanyabiashara wadogo wadogo nchini ikiwa ni jitihada za Serikali katika kukusanya mapato nchini.
Akizungumzia mipango hiyo leo, Jijini Dar es Salaam, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) Alphayo Kidata amesema wameamua kuanza kugawa mashine hizo kwa wafanyabiashara wadogowadogo ambao wengi wao hawana uwezo wa kugharamia manunuzi ya mashine hizo.
“ Mamlaka imeona changamoto wanayoipata wafanyabiashara wadogo hivyo imeamua kuanza kugawa mashine hizi ili kuondokana na tatizo la kutotoa risiti za mauzo kwa wafanyabiashara hao ambao walio wengi walikuwa na kisingizio cha kutokuwa na mashine hizo”. Alisema Kidata.
Kamishna Kidata ameongeza kuwa Mamlaka yake imeshaagiza mashine hizo na zipo tayari kuanza kugawiwa mwezi huu kwa wafanyabiashara  hao ikiwa ni awamu ya kwanza ya ugawagaji wa mashine hizo ambao utafanyika nchi nzima.
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeazimia kugawa mashine laki mbili kwa wafanyabiashara wadogo wadogo nchini ikiwa ni jitihada za kuweza kukusanya mapato yatokanayo na kodi za biashara kwa urahisi na ufanisi mkubwa.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.