MAFUNZO KWA ASKARI WA CHUO CHA MAFUNZO ZANZIBAR

 Kaimu Mkurugenzi Tume ya Taifa ya Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya Zanzibar
Dkt. Mahmoud Ibrahim Mussa akitoa mafunzo juu ya kuwasaidia watumiaji wa madawa
ya kulevya kwa Askari wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar katika ukumbi wa Chuo hicho Kilimani
Mjini Zanzibar.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya kuwasaidia watumiaji wa madawa ya kulevya wakimsikiliza
Kaimu Mkurugenzi Tume ya Taifa ya Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya Zanzibar
Dkt. Mahmoud Ibrahim (hayupo pichani) katika mafunzo ya siku moja yaliyofanyika
ukumbi wa Chuo hicho.
Picha na Haji Ramadhan Suweid.
———————————————————————————————————————-
Na Miza kona – Maelezo Zanzibar                 
Matumizi ya dawa za kulevya ni janga linaloathiri vijana na kupoteza mwelekeo ambao hupelekea kufanya maamuzi yasiyo sahihi na kupoteza kumbukumbu jambo ambalo linarejesha nyuma maendeleo ya Taifa. 
Akitoa mafunzo kwa watendaji wa Chuo cha Mafunzo  Kaimu Mkurugenzi Tume ya Taifa ya Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya
Kulevya Dkt Mahmoud Ibrahim Mussa katika shamra shamra za kuadhimisha siku ya kudhibiti madawa ya kulevya.
Amesema mtumiaji wa madawa ya kulevya huathirika ubongo ambao hawezi kuacha kutumia madawa hayo kwa kuongeza kiwango hali ambayo inayopelekea kutoweza kufanya shughuli za kimaendeleo.
Ameeleza kuwa maambukizi makubwa ya virusi vya ukimwi yanasababishwa zaidi na watumiaji wa madaya ya kulevya kwa njia ya kujidunga sindano ambayo yanaathiri jamii na kupoteza nguvu ya taifa.
“Sigara ina madhara makubwa nacho pia ni kilevi  ina kemikali 4000 ambayo huleta madhara kwa binadamu na kuharibu viungo,
husababisha maradhi ya moyo, kansa pia hupelekea ugonjwa wa akili,” alitanabahisha Dkt Mahamoud. 
Amefahamisha jamii itanabahishwe zaidi juu ya madhara ya matumizi dawa za kulevya pamoja na
uvutaji wa sigara jinsi ya kuyaepuka na  na kuwasaidia watumiaji wa madawa ya kulevya ili  kuweza kuyaacha madawa hayo.
Dkt Mahamoud amefahamisha kuwa kinga ya msingi ya kuachana matumizi ya dawa za kulevya imo ndani ya familia ambayo iweze kumkubali muathirika ili aweze kuachana na kilevi kwa kumpa huduma nzuri bila ya kunyanyapaa.
Aidha wameshauri kutafuta njia ya kuweza kudhibiti utumiaji wa dawa za kulevya katika Vyuo vya mafunzo kwa wafungwa kwani imebainika kuwa baadhi yao hutumia dawa hizo wakati wanatumia kifungo.    
Nao washiriki wa mafunzo hayo wameiomba jamii kutoa mashiriakiano makubwa na vyombo vya kudhibiti madawa ya kulevya ili kuweza   kuwafichua na kuwadhibiti wale wote wanaoingiza, wanaosambaza na watumiaji pamoja na kutoa elimu hiyo kupitia skuli mbali mbali ili kuhakikisha kuwa jambo hilo linadhibitiwa nchini.
Aidha wameitaka Tume ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya kuwa huru katika kutoa huduma zake ii iweze kufanyakazi kwa uwazi pamoja na wazazi kuwafundisha watoto wao maadili mema na kukua katika misingi mizuri kwani vishawishi vya madhara hayo ni vijana.
Mafunzo hayo ni ya siku moja ambayo yaliyowashirikisha watendaji wa Chuo cha Mafunzo ambapo
kilele chake kinatarajiwa kufanyika tarehe 26 mwezi huu. 
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

LICHA YA UZURI WAKE MWANADADA ELIZABETH MICHAEL a.k.a LULU SI MALI KITU MBELE YA RAY, AMKWEPA KUOGOPA AIBU.

ANGALIA PICHA NDEGE KUBWA YA ABIRIA DUNIANI ILIYOANZA SAFARI NDEFU ZAIDI!

ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA NDANI YA CHAKE CHAKE,MKOA WA KUSINI PEMBA LEO.

IJUE HISTORIA YA UHASIMU WA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI

NCHI YA URUSI NDIYO NCHI INAYOONGOZA KWA KUWA NA UBORA WA ELIMU NA VYUO DUNIANI.

TFF YATANGAZA MAJINA YA WACHEZAJI 30 WATAKAOWANIA TUZO YA MCHEZAJI BORA MSIMU HUU

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA