MASAUNI AFANYA ZIARA MKOANI GEITA, ATEMBELEA KITUO CHA POLISI KILICHOLALAMIKIWA BUNGENI


 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na mamia ya wananchi wa Kijiji cha Nyakabale, Kata ya Mgusu, mkoani Geita ambao ni majirani wa Kampuni ya Uchimbaji wa Dhahabu ya GGM mkoani humo. Wananchi hao wamelalamika kuwepo na vitendo vya ukatili dhidi yao vinavyofanywa na baadhi wa askari wa kampuni hiyo. Hata hivyo Mhandisi Masauni aliwataka Polisi mkoani humo kufanya uchunguzi wa haraka dhidi ya tuhuma hizo.
 Mkazi wa Kijiji cha Nyakabale, Kata ya Mgusu, mkoani Geita, Biosi Makongoro akitoa kero yake kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto aliyekaa) dhidi ya Kampuni ya Uchimbaji wa Dhahabu ya GGM mkoani humo
ambayo ipo jirani na kijiji hicho, kuwa askari wa kampuni hiyo wanadaiwa kuwanyanyasa wananchi hao wanapopita katika eneo la Kampuni hiyo. Hata hivyo Mhandisi Masauni aliwataka Polisi mkoani humo kufanya uchunguzi wa haraka dhidi ya tuhuma hizo.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akiwasili Kituo cha Polisi Runzewe kilichopo Kata ya Uyovu wilayani Bukombe ambacho Mbunge wa Jimbo hilo, Dotto Biteko aliuliza swali la nyongeza Bungeni hivi karibuni akisema kituo hicho kinahitaji matengenezo makubwa na kumuomba Naibu Waziri huyo kufanya ziara jimboni kwake kujionea kituo hicho. Hata hivyo, Masauni alisema Serikali yake itahakikisha kituo hicho kitakuwa katika hali nzuri.
 Mkuu wa Kituo cha Polisi Runzewe kilichopo Kata ya Uyovu wilayani Bukombe, Jackson Kirahuka akimuonyesha Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto aliyevaa koti) sehemu mbalimbali za kituo hicho ambacho Mbunge wa Jimbo la
Bukombe, Dotto Biteko (katikati) aliuliza swali la nyongeza Bungeni hivi karibuni akisema kituo hicho kinahitaji matengenezo makubwa na kumuomba Naibu Waziri huyo kufanya ziara jimboni kwake kujionea kituo hicho. Hata hivyo, Masauni alisema Serikali yake itahakikisha kituo hicho kitakuwa katika hali nzuri. Aliyevaa Kaunda suti ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Amani Mwenegoha.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wa pili kushoto) akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Meja Jenerali, Mstaafu Ezekiel Kyunga (meza kuu), Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini, Joseph Msukuma (kulia), na Mkuu wa Jeshi la Polisi mkoani humo, Mponjoli Mwabulambo, wakati Naibu Waziri huyo alipofanya ziara ya kikazi mkoani humo.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akimfafanulia jambo Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini, Joseph Msukuma (watatu kulia), na Mkuu wa Jeshi la Polisi mkoani humo, Mponjoli Mwabulambo (wapili kushoto), wakati Naibu Waziri huyo alipofanya ziara ya kikazi mkoani humo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akitoka ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bukendo, Amani Mwenegoha (kushoto) mara baada ya kumaliza kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hiyo iliyopo mkoani Geita. Naibu Waziri alifanya ziara ya kikazi mkoani Geita. 
 Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

ANGALIA PICHA NDEGE KUBWA YA ABIRIA DUNIANI ILIYOANZA SAFARI NDEFU ZAIDI!

LICHA YA UZURI WAKE MWANADADA ELIZABETH MICHAEL a.k.a LULU SI MALI KITU MBELE YA RAY, AMKWEPA KUOGOPA AIBU.

ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA NDANI YA CHAKE CHAKE,MKOA WA KUSINI PEMBA LEO.

IJUE HISTORIA YA UHASIMU WA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA

NCHI YA URUSI NDIYO NCHI INAYOONGOZA KWA KUWA NA UBORA WA ELIMU NA VYUO DUNIANI.

TFF YATANGAZA MAJINA YA WACHEZAJI 30 WATAKAOWANIA TUZO YA MCHEZAJI BORA MSIMU HUU