Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akipokea mwenge wa Uhuru kutoka kwa mkuu mkuu ya Mufindi Bw Jowika Kasunga leo baada ya kuanza mbio zake wilaya ya Mufindi |
Mbio za Mwenge katika Halmashauri ya Iringa |
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard kasesela wa tatu kulia akisakata dansi katika mapokezi ya Mwenge Iringa |
HALMASHAURI za wilayani nchini zimetakiwa kutenga pesa za makusanyo ya ndani kwa ajili ya kuwasaidia vijana asilimia tano ya makusanyo hayo ili kutumika kuwakomboa vijana kiuchumi .
Rai hiyo imetolewa leo na kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa, George Mbijima wakati wa mkesha wa mbio hizo mwenge kijiji cha Ifunda katika halmashauri ya wilaya ya Iringa .
Alisema kuwa jukumu ya Halmashauri kutenga asilimia 5 ya makusanyo yake ya mapato ya tayari serikali imeagiza kufanya hivyo na ni vema kila Halmashauri kuhakikisha inatenga fedha hizo kwa ajili ya vijana ikiwa ni pamoja na kuwatengea ardhi kwa ajili ya kufanyia shughuli za kiuzalishaji .
Mbijima alisema “rai yangu kwenu vijana ni kutoa nguvukazi kwa kushiriki kwa moyo thabiti katika kazi za ujenzi wa miradi ya maendeleo. Kufanya hivyo kutasaidia kuharakisha ukamilishaji wa miradi hiyo. Aidha, nawapongeza kwa utayari wenu kwa mradi huu wa maji na kuchangia asilimia 2.5 ya gharama za mradi huu wa maji”.
Kiongozi huyo aliwahakikishia wananchi wa vijiji hivyo kuwa Ofisi ya Rais, Tawaala za Mikoa na Serikali za Mitaa pamoja na Halmashauri ya wilaya ya Iringa zitaendelea kutafuta fedha za kukamilisha mradi huo muhimu.
Alisema lengo la Serikali ni kuendelea kusogeza huduma ya maji kwa wananchi kama Sera ya Maji ya mwaaka 2002 inavyoelekeza.
Huku akiwataka vijana kuacha kutumia fedha hizo za mikopo kuongeza wake ama kufanyia anasa zisizo na tija katika maisha yao.
Alisema Miradi mbali mbali ambayo imezinduliwa kwa ajili ya vijana ukiwemo mradi wa kilimo kwa kijiji cha Usengelendeti kwa ajili ya kikundi cha vijana wa Nguvu kazi ambao wanafanya shughuli ya kilimo ni moja kati ya miradi itakayowakomboa vijana iwapo watatimiza wajibu wao.
Akisoma risala ya utii kwa Rais wa Dr John Magufuli wakati wa hitimisho ya mbio hizo kwenye halmashauri ya wilaya ya Iringa mkuu wa wilaya ya Iringa Bw Richard Kasesela alisema kuwa katika kuwajali vijana jumla ya mikopo kwa vikundi vya vijana vya kijasiliama mali vikundi 38 vimepatiwa mikopo yenye thamani ya Tsh milioni 60.2 kwa ajili ya vikundi zimetolewa kati ya fedha hizo Tsh milioni 37.5 zilitokana na asilimia 5 ya mapato ya ndani na Tsh milioni 17.7 zilitokana na mfuko wa vijana wa Halmashauri huku Tsh .milioni 5 iliokana na mkopo wa wizara ya habari ,vijana utamaduni na michezo.
Comments