WAZIRI MWIGULU NCHEMBA ATAKA RAIS DR MAGUFULI AOMBEWE..



Waziri  wa  kilimo ,Mifugo na uvuvi Bw Mwigulu Nchemba akizindua  tamasha la urafiki katika  viwanja  vya Ndege mjini Morogoro jana Juni 2 ,tamasha  lililoandaliwa na ushirikiano wa makanisa katika mkoa  wa Morogoro na kuongozwa na mhubiri wa  kimataifa toka nchini Canada Dr Peter  Youngren
Mkuu  wa  mkoa  wa Morogoro Dkt. Kabwe Steven Kabwe kulia  na  waziri wa Kilimo ,Mifugo na Uvuvi wakiwapungia  wananchi wa Morogoro mikono  wakati  wakiwasili katika  viwanja vya Ndege kwa ajili ya uzinduzi wa tamasha  la Urafiki lililoanza jana  Juni 2 hadi Jumapili Juni 5
Waziri  wa  kilimo ,Mifugo na uvuvi Bw Mwigulu Nchemba ambae ni mbunge wa  jimbo la Iramba akiwapungia mikono  wananchi wa Morogoro  wakati  akiwasili katika  viwanja  vya Ndege  kuzindua tamasha la Urafiki
mhubiri wa  kimataifa toka nchini Canada Dr Peter  Youngren ambae  anaongoza  tamasha  la Urafiki mjini Morogoro akimpongeza waziri wa Kilimo ,Mifugo na Uvuvi Bw Mwigulu Nchemba  baada ya  kuwasili mkoani Morogoro  kuzindua tamasha   hilo
Waziri Nchemba  akimsikiliza mhubiri wa  kimataifa toka nchini Canada Dr Peter  Youngren
mhubiri wa  kimataifa toka nchini Canada Dr Peter  Youngren akiwa katika  picha ya pamoja na waziri  wa kilimo ,Mifugo na Uvuvi Bw Mwigulu Nchemba 
Waziri  Nchemba  akipokelewa na RC Morogoro Dkt. Kabwe Steven Kabwe
Waziri Nchemba  akiwasili  uwanja  wa mkutano
mhubiri wa  kimataifa toka nchini Canada Dr Peter  Youngren wa  pili  kushoto  akiwa na waziri wa kilimo ,Mifugo na Uvuvi Mwigulu Nchemba pamoja na viongozi waandaaji wa tamasha la Urafiki Morogoro  kushoto wa kwanza ni Askofu wa kanisa la  Philndelphia Dr Yohana Masingu
mkuu  wa mkoa wa Morogoro Dkt. Kabwe Steven Kabwe kulia akiwa na waziri Nchemba
Mkuu wa  mkoa wa Morogoro Dkt. Kabwe Steven Kabwe kulia akimwongoza waziri Nchemba
mhubiri wa  kimataifa toka nchini Canada Dr Peter  Youngren akiteta  jambo na  waziri Nchemba
Mapokezi ya waziri Nchemba Morogoro
Kwaya  ikitumbuiza katika uwanja  huo
Waziri Nchembe  akizindua tamasha   hilo
W
mhubiri wa  kimataifa toka nchini Canada Dr Peter  Youngren akiendelea  kuhubiri
Wananchi  wakiwa katika  viwanja  hivyo
Mtoto  ambae  alikuwa hasikii toka azaliwe  akijaribiwa baada ya kuombewa na kupona
Mwanamke  aliyekuwa kapooza akitembea  baada ya maombi
Mmoja kati ya  watu  walioanguka kwa mapepo  uwanjani wakati wa maombi


Mkazi  wa Morogoro  aliyekuwa anatembea kwa  shida baada ya kuotwa na uvimbe mkubwa eneo la siri akiruka  ruka kwa furaha  baada ya kuombewa na kupona na mhubiri wa  kimataifa toka nchini Canada Dr Peter  Youngren
Mwanamke  ambae  alikuwa  na matatizo  ya  kusikia kwa miaka  zaidi ya 15 akitoa  ushuhuda  baada ya  kuombewa na mhubiri wa  kimataifa toka nchini Canada Dr Peter  Youngren kushoto
mhubiri wa  kimataifa toka nchini Canada Dr Peter  Youngren akihubiri  katika tamasha    la Urafiki mjini Morogoro 



“ Tunapokusanyika na  tunapokuwa  faragha katika ibada  zetu tuliombee taifa  letu ……jambo la pili kwa  uzito  huo  huo tumwombee Rais  wetu mpendwa Dr John Magufuli  kazi anayoifanya ni ngumu … kazi anayoifanya ni kwa  niaba ya watanzania  wote na utashi  ule anaoendanao ninyi  wenyewe  mliomba  sana kabla ya kumpigia kura ….uzoefu  unaonyesha mabadiliko  huwa  hayaji rahisi  rahisi  adui  huwa hakubali  kushindwa kirahisi kwa  hiyo  kila tunapoongea na Mungu  wetu  tukumbuke  kumwombea Rais wetu ili kila mema anayoliwazia Taifa  yaweze  kutimia” alisema  waziri Nchemba 
Kuwa kwa upande  wake kila anapoona  watumishi  wa Mungu  wakiwa wamekusanyika kwa ajili ya huduma huwa haachi  kuwasogelea  japo kushikana nao mikono kama sehemu ya  kupokea baraka  kutoka kwao kwani  wapakwa mafuta  wakisema  tu ubarikiwe Mungu juu mbinguni  huweka tiki ya baraka.
“Na hivyo   ndivyo  nilivyopata hata  ubunge nilikuwa  sina  gari wala baiskeli  na  wazazi  wangu  walikuwa wanaishi katika  nyumba  ya tembe wakiwa na maisha magumu  nikaenda kanisani  kulikuwa na Harambee japo  sikuwa na pesa  nyingi  niliamua  kuchangia  kidogo  tu  …..watumishi  wale  wakasema  Ee Mungu mjalie haja ya moyo wake  huyu kijana na mimi nilikuwa  nikiwaza ubunge kweli ubunge  ukatiki …..na  hivi  leo amekuja mhubiri wa  kimataifa toka nchini Canada Dr Peter  Youngren akasema kwa  lugha ya kiingereza  kuwa Ee Mungu timiza  ndoto ya  kijana  huyo na mimi ndogo  hiyo inaendelea  kuota  hivyo  hivyo kwa  hiyo najua na ninyi mtanikumbuka katika majukumu ambayo nimepewa na Rais   ……leo baada ya saa 4 asubuhi hatukuwa na ratiba ya vikao  vya bunge  nimelazimika kuja Morogoro kuifanya kazi hii na leo hii nitageuza bungeni “
Kwani  alisema majukumu ambayo anayatumikia pia yana harufu  ile ile  ya ambayo amewaomba  kuzidisha  maombi  kuliombea  Taifa kwani yana harufu ya umwagaji  wa damu .
 Alisema  waziri Nchemba  kuwa alipoteuliwa na Rais Dr Magufuli kabla  hata ya kuapishwa alipata  taarifa ya mifugo  kuuwawa na   watu  kuchinjana kwa kukatana mapanga mkoani Morogoro  ambayo  yalimkumbusha mapigano ya  chuki na wivu kwa  Abeli na Kaini mmoja akiwa mkulima na mwingine mfugaji .

“ Tuliombee Taifa  letu  kila mmoja afanye kazi inayomlete kipato  pasipo kuwa na wivu na  bila kuwa na dharau kwa kazi  ya mwenzake ….kila  nikipita  huwa nawaeleza   watumishi wangu  kuwa hakuna mali ,mifugo,shamba  ama kitu chochote  chenye dhamani  kubwa  kuliko uhai wa mwa  wanadamu”
Kuwa  serikali  itatengeneza mazingira  bora  ya wakulima ama  wafugaji  kufanya kazi  zao kwa uhuru na amani japo  kila  mmoja anapaswa  kutambua  kuwa uhai ni zaidi ya yote.
Kwa  upande wake mhubiri wa  huyo  kimataifa toka nchini Canada Dr Peter  Youngren limpongeza waziri Nchemba  kwa  kujiweka  mbele katika huduma&nbs ...

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

ALLY KAMWE AZIMIA KWA MKAPA.

RAIS SAMIA KUZINDUA MKUTANO MKUU WA 79 WA BARAZA LA MICHEZO YA MAJESHI DUNIANI

MIGINGO KISIWA KIDOGO ZAIDI AFRIKA KILICHOGOMBEWA NA UGANDA, KENYA