KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
Simu:
255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Faksi: 255-22-2113425
|
OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK
OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa kifungu cha 48 cha sheria
ya tafsiri za sheria (Interpretation of
Laws Act) Sura 1, leo tarehe 5
Julai, 2016 ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Maendeleo ya TIB
Prof. William Lyakurwa.
Kufuatia hatua
hiyo, kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo chini ya kifungu cha 9 (2) cha ya Sheria
ya mashirika ya umma (Public Corporations
Act) Sura 257, Mhe. Rais amemteua Prof.
Palamagamba J. A. M. Kabudi (pichani)kushika nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Benki
ya Maendeleo ya TIB kwa kipindi cha miaka mitatu.
Kufuatia mabadiliko
hayo, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango kwa mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa kifungu cha
48 cha sheria ya sheria ya tafsiri za sheria (Interpretation of Laws Act) Sura 1,
ametengua uteuzi wa Wajumbe Bodi ya Benki ya Maendeleo ya TIB.
Aidha, kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo
chini ya kifungu cha 9 (1) cha ya Sheria ya mashirika ya umma (Public Corporations Act, Sura 257) Mhe.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango ameteua wajumbe wapya wa
Bodi wafuatao kwa kipindi cha miaka mitatu:
1.
Brig. Gen (Rtd) Mabula Mashauri
2.
Dkt. Razack B. Lokina
3.
Bi. Rose Aiko
4.
Prof. Joseph Bwechweshaija
5.
Bw. Said Seif Mzee
6.
Dkt. Arnold M. Kihaule
7.
Bw. Maduka Paul Kessy
8.
Bw. Charles Singili
Uteuzi wa Mwenyekiti na Wajumbe wapya wa Bodi
unaanza tarehe leo 5 Julai, 2016.
Gerson Msigwa
Comments