SAMATTA AFUNGA MFULULIZO GENK IKIUA 5-0, 3-0 NDANI YA SIKU MBILI

Na Mwandishi Wetu, GENK
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania ameendelea kung'ara katika klabu yake, KRC Genk ya Ubelgiji baada ya kufunga mabao mfululizo ndani ya siku mbili katika mechi za kirafiki za kujiandaa na msimu mpya.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Simba SC, juzi alifunga bao moja katika ushindi wa 3-0 juzi dhidi ya ESK Leopoldsburg nyumbani.
Samatta alifunga bao la kwanza dakika ya 20 Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk, wakati mabao mengine yalifungwa na Karelis dakika ya 29 na Walsh dakika ya 66.
Kabla ya hapo, Samatta alifunga pia katika ushindi wa 5-0 kwenye mchezo mwingine wa kirafiki wiki ugenini dhidi ya Bocholt Julai 1. 
Nyota ya Mbwana Samatta (kulia) meendelea kung'ara Ulaya

VIDEO; SAMATTA ALIVYOFUNGA GENK IKIUA 5-0, 3-0Samatta alifunga dakika ya 68 likiwa bao la nne, wakati mabao mengine yamefungwa na Kebano dakika ya 15, de Camargo dakika ya 45 yote kwa penalti, Trossard dakika ya 47 na Heynen dakika ya 88.
Kabla ya mechi hiyo ya Julai 1, Samatta aliichezea pia Genk katika mchezo wa kirafiki Juni 25, ikishinda 7-1 dhidi ya Unity Termien.
Lakini siku hiyo, Samatta hakufunga na mabao ya timu yake yalifungwa na de Camargo, Dewaest, Kebano, Sabak, Van Zeir, Karelis na Pozuelo huku la wapinzani wao likifungwa na Baur.  
Genk watashuka tena dimbani Julai 7 kumenyana na Lommel, Julai 9 na Lierse na Julai 17 na FC Eindhoven.
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

LICHA YA UZURI WAKE MWANADADA ELIZABETH MICHAEL a.k.a LULU SI MALI KITU MBELE YA RAY, AMKWEPA KUOGOPA AIBU.

IJUE HISTORIA YA UHASIMU WA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA

PICHA:NYOKA AINA YA CHATU AUWAWA KANISANI BAADA YA KUKUTWA NYUMBANI KWA MFANYABIASHARA MAARUFU JIJINI ARUSHA AKISADIKIWA KWA IMANI ZA KISHIRIKINA

WENGI WAJITOKEZA KUMUAGA MPENDWA WAO MWANAHABARI JOYCE MMASI