MAALIM SEIF AWASILI ZANZIBAR AKITOKEA MAREKANI


 Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF Maalim Seif Sheriff Hamad akiwapungia mkono baaadhi ya wananchama waliofika uwanja wa ndege zanzibar kumpokea akitokea Marekani.
Maalim Seif Shari Hamad ambaye ni Katibu Mkuu wa Chama cha wananchi CUF akisalimiana na baadhi ya viongozi waliofika uwanja wa ndege wa Kimataifa  Abeid Aman Karume kumpokea. (Picha na Talib Ussi).

Na Talib Ussi, Zanzibar
Katibu Mkuu wa chama cha wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad amerejea Nchini leo akitokea katika ziara zake za Ughaibuni  amewataka wanachi na wanachama wa chama hicho  kuendelea  kuwa na subra.

Maalim ameyaeleza hayo nyumbani kwake wakati akitoa salamu kwa wananchgama waliokua kusanya hapo na kuomba kuelezwa chochote.

“Tumekutana na watu muhimu katika safari yetu na imekuwa na mafanikio makubwa lakini ni mapema kuwaeleza nini kinaendelea” alieleza Maalim Seif.

Alisema kuwa katika safari yake hiyo amepokewa vizuri na kueleza matatizo ya kubakwa kwa demokrasia Zanzibar  na wote aliokutana nao alidai wamemfahamu.

“Ni vyema tukaendelea kuwa subra huku mambo yetu yakifuatiliwa kwa karibu mnoo” alieleza Maalim Seif.
Malim Seif alifika Kiwanja cha ndege Zanzibar munamo saa 11;30n za jioni akiongozana na wajumbe ujumbe wake na walinzi wake waliandamana katika ziara yake hiyo.

Mapema baadhi ya viongozi wa chama hicho walifika kiwan jani hapo kwa ajili ya kumpokea wakiongozwa na aliyekuwa Mgombea mwenza wa Ukawa Juma Duni Haji.

Akimkaribisha Maalim Seif Mkurugenzi wa Habari na Uenezi CUF Salim Biman alimueleza maalimu kwamba wanancha leo walijipanga kuja kumpokea mapokezi makubwa lakini alidai waliwazuia.

“Tumewaambia muda ukifika watakuja kumpokea kwa kishindo lakini kwanza watulie” alieleza Biman
Katika ziarav hiyo Maalim Seif alienda Uengereza, Ubeligiji, Uholanzi na baadae kuhudhuria mkutano Mkuu wa chama cha Democratic wa kumteua mgombea wao Hilary Clinton huko Marekani.
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

ANGALIA PICHA NDEGE KUBWA YA ABIRIA DUNIANI ILIYOANZA SAFARI NDEFU ZAIDI!

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

LICHA YA UZURI WAKE MWANADADA ELIZABETH MICHAEL a.k.a LULU SI MALI KITU MBELE YA RAY, AMKWEPA KUOGOPA AIBU.

IJUE HISTORIA YA UHASIMU WA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI

KWA HERI KAMANDA WETU ABBAS KANDORO

YANGA SC WAANZA KAZI AFRIKA LEO…WANAKIPIGA NA U.S.M. ALGER SAA 4:00 USIKU ALGERIA

NCHI YA URUSI NDIYO NCHI INAYOONGOZA KWA KUWA NA UBORA WA ELIMU NA VYUO DUNIANI.

DC MJEMA AONJA ADHA YA MAFURIKO AKIKAGUA ATHARI ZA MAFURIKO ILALA