SAMATTA APELEKWA CROATIA EUROPA LEAGUE

Na Mwandishi Wetu, NYON
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta atakutana na Lokomotiva Zagreb ya Croatia katika hatua ya mwisho ya mchujo wa kuwania hatua ya makundi ya Europa League.   
Droo ya Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA) iliyopangwa leo mjini Nyon, Uswisi KRC Genk ya Ubelgiji itamenyana na Lokomotiva Zagreb ya Croatia. 
Mechi ya kwanza itachezwa Alhamisi Agosti 18 mjini Zagreb na marudiano yatakuwa Alhamisi ya Agosti 25 Uwanja wa Luminus Arena, Genk.
Mbwana Samatta (katikati) akifurahia na wachezaji wenzake wa KRC Genk
Samatta na Genk wakifuzu mtihani huo, wataingia moja kwa moja kwenye hatua ya makundi, ambako vigogo mbalimbali wa Ulaya huanzia hatua hiyo.
Samatta usiku wa jana alicheza vizuri Uwanja wa Turner's Cross, mjini Cork, Ireland na kuiwezesha KRC Genk kushinda 2-1 ugenini dhidi ya Cork City FC ya Ireland.
Na Genk inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 3-1, baada ya wiki iliyopita kushinda 1-0 mjini Genk.
Mabao ya Genk jana yalifungwa na Thomas Buffel dakika ya 12 na Sebastien Dewaest dakika ya 41, wakati la wenyeji lilifungwa na Alan Bennett dakika ya 63.
Na Samatta aliyewekewa ulinzi mkali na mabeki wa Cork City FC, alicheza kwa dakika 77 kabla ya kumpisha Bryan Heynen kumalizia mechi hiyo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.