TAARIFA ZA MANJI KUACHIA NGAZI, MZEE AKILIMALI ASEMA AMEITWA KUYAMALIZA

Wakati sekeseke la Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji kudaiwa kujiuzulu nafasi yake hiyo, mwanachama mkongwe wa klabu hiyo, Ibrahim Omary Akilimali maarufu kwa jina la Mzee Akilimali ametoa kauli tata juu ya sakata hilo.
 



 Wakati huu ambapo Manji hatatoa tamko lolote juu ya uamuzi wake huo wa kujiuzulu, Mzee Akilimali amenukuliwa akisema kuwa kuna watu wa Yanga wamemuita ili kuzungumza kuumaliza mvutano unaoendelea ambapo inaelezwa kuwa mzee huyo amechangia maamuzi ya Manji kujiondoa Yanga kutokana na kumshutumu kwa maneno mengi.

Akihojiwa na kituo cha Radio ha EFM, muda mfupi uliopita Mzee Kilimali alinukuliwa akisema: “Msitake kuyakuza haya mambo, subirini kwanza nataka tuyamalize, mimi wameniita ndiyo maana nipo huku ili kuyamaliza.”

Alipoulizwa yupo wapi na ameitwa na nani, Akilimali alisema: “Nimekwambia nimeitwa huku, wewe subiri kwanza tuyamalize kisha utanipigia, subiri baada ya nusu saa nitakubeep unipigie.”
 
Licha ya kuendelea kubanwa kufafanua zaidi juu ya kinachoendelea, mzee huyo alisisitiza kuwa pigiwe baadaye na kukata simu.

Mzee Akilimali ni mzaliwa wa Kigoma, ambapo anadai alianza kuipenda Yanga tangu miaka ya 1950.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.