TAASISI ZATAKIWA KUANZISHA MFUMO WA KUPIMANA

2Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe Lt. Mstaafu Chiku Galawa (Kulia) wakati alipotembelea ofisini kwake kupata taarifa ya hali ya miundombinu katika mkoa huo.
4Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Meneja wa wakala wa barabara nchini (Tanroads) mkoa wa Mbeya Eng. Paul Lyakurwa wakati alipokagua barabara ya Ikana-Makamba –Chitete iliyopo mkoa wa Songwe.
5Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akikagua kituo cha kukuza mawimbi ampilification station kilichopo miangalau mkoani Rukwa. Kulia kwake ni Meneja wa kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Mkoa wa Katavi na Rukwa Bw. Peter Kaguru.
6Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Zelothe Stephen akitoa taarifa ya hali ya Miundombinu katika mkoa huo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakati alipomtembelea ofisini kwake.
7Meneja wa Wakala wa barabara nchini (Tanroads) Mkoa wa Rukwa Eng. Masuka Mkina (wa pili kushoto) akisoma taarifa ya utendaji ya taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa Waziri Profesa Makame Mbarawa wakati alipofanya mazungumzo na viongozi wa taasisi hizo.
8Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa pili kulia) akizungumza na viongozi wa taasisi zilizo chini ya yake (hawapo pichani), wakati alipokutana nao Mkoani humo.
9Viongozi wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mkoani Rukwa, wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani) wakati alipokutana nao Mkoani Rukwa.
……………………………………………………………………………………….
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amezitaka taasisi zilizo chini ya Wizara yake kuanzisha mfumo maalumu wa makubaliano utakaotumika kupima utendaji kazi wa watumishi ili kuweza kufikia malengo yaliyokusudiwa na kutoa matokeo chanya.
Waziri Mbarawa ameyasema hayo Mkoani Rukwa alipofanya mazungumzo na Viongozi na watendaji wa taasisi hizo wakati alipotembelea mkoa huo kwa lengo la kukagua hali ya miundombinu na kuwaeleza mtazamo mpya wa Serikali ya Awamu ya Tano.
Amesema katika mfumo huo Waziri ataingia mkataba na wenyeviti wa bodi wakati Katibu Mkuu wa kila sekta kuingia mkataba na watendaji wakuu wa taasisi hizo na watendaji hao wataingia mikataba na wafanyakazi wao ili kuweza kuweka mazingira ya kila mfanyakazi kufikia malengo yaliyowekwa na wizara pamoja na taasisi husika.
“Mimi nitawekeana mkataba na wenyeviti wa bodi za taasisi zote, kwa Sumatra moja ya vipengele vitakavyokuwa kwenye  mkataba huo ni pamoja na mkakati madhubuti wa  kupunguza ajali za barabarani zinazosababisha  vifo kwa Watanzania, TCRA Makusanyo kwenye makampuni ya simu na taaasisi nyingine hivyo hivyo”, amesema Prof. Mbarawa.
Aidha, Waziri Mbarawa amehimiza taasisi hizo kufanya kazi kwa bidii ili kuwajengea miundombinu iliyo bora watanzania ili kuweza kuwafikisha katika uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
Aidha,  Profesa Mbarawa amewataka watendaji hao kufanya kazi kwa ubunifu, kasi na uadilifu ili kuweza  kutatua changamoto zinazowakabili wananchi na kuwajibika kwa ajili ya maslahi ya wananchi na kubadili maisha ya watanzania kwa ujumla.
“Ni wakati wa kutekeleza kauli mbiu ya hapa kazi tu kwa vitendo, hivyo nawataka muwe wabunifu katika utendaji kazi za kila siku na muweze kutoa matokeo chanya ya haraka kwa wananchi”, amesisitiza Prof. Mbarawa.
Awali akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Songwe Lt. Mstaafu Chiku Galawa, Profesa Mbarawa amesema Serikali kupitia wizara yake itaendelea kupandisha hadhi baadhi ya barabara zilizo chini ya Halmashauri na kuwa chini ya Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), ili kuweza kuendelea kuboresha hali ya miundombinu na kuunganisha mkoa huo na Mikoa ya Mbeya, Rukwa pamoja na nchi zinazozunguka mikoa hiyo kwa barabara za lami.
Profesa Mbarawa amemuhakikishia Mkuu wa Mkoa huyo kuwa Serikali itaendelea kufanya matengenezo kwa barabara zote nchini kupitia gawio kutoka Mfuko wa Barabara nchini (Road fund) ili kuinua uchumi wa Mkoa.
Waziri Mbarawa yupo katika ziara ya kukagua utendaji kazi kwa wafanyakazi pamoja na hali ya Miundombinu katika mikoa ya nyanda za juu kusini.
Imetolewa na kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI