DC MUHEZA APIGA MARUFUKU BODABODA KUENDESHWA ZAIDI YA SAA SITA


Mkuu wa wilaya ya Muheza Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza na bodaboda wa wilaya hiyo ambapo alikutana nao na kuzungumza nao kwenye uwanja wa Jitegemee wilayani humo ambapo alipiga marufuku kuendeshwa usiku zaidi ya saa sita.

Katibu Tawala wa wilaya ya Muheza (Das) akizungumza katika mkutano huo kabla ya kumkaribisha Mkuu wa wilaya hiyo,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo aliyekaa kushoto na anayefuata ni Mwenyekiti wa Waendesha Boda Boda wilayani Muheza
 
 Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Muheza ambaye pia ni Afisa Biashara wa wilaya hiyo,Ally Mokiwa akielezea namna walivyojipanga kuhakikisha waendesha bodaboda hao wanakata leseni za kuendesha shughuli zao katikati ni Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo
wa pili kutoka kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Muheza, Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo akimsikiliza kwa umakini Mkuu wa Usalama Barabarani wilayani Muheza(DTO) Herbert Kazonde wakati wa mkutano huo na waendesha bodaboda uliofanyika kwenye uwanja wa Jitegemee wilayani humo kulia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Muheza.


Katibu wa Chama cha Waendesha Boda Boda wilayani Muheza,Francis Gerald akizungumza katika mkutano huo kuhusu changamoto ambazo zinawakabili


Baadhi ya waendesha bodaboda wilayani Muheza wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo alipokuwa akizungumza nao kusisitiza umuhimu wa wao kutii sheria za usalama barabarani ikiwemo kuacha kufanya vitendo vya uhalifu


 Baadhi ya Bodaboda zikiwa zimepaki kwenye uwanja wa Jitegemee wilayani Muheza huku madereva wakiwa kwenye kikao chao na Mkuu wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga, Mhandisi,Hajat Mwanasha Tumbo.
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.