MALINZI AWAPELEKA SERENGETI BOYS SHELISHELI


Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi kwa mara nyingine ametimiza ahadi yake kwa kuipeleka nje ya nchi timu ya taifa ya Tanzania ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ ambako itapiga kambi ya utulivu kabla ya kucheza na Congo-Brazzaville katika mechi ya mkondo wa kwanza kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri huo.
Benchi la ufundi lilimshauri Rais Malinzi kwamba kambi hiyo ipigwe jijini Victoria, kwenye Kisiwa cha Mahe nchini Shelisheli. Serengeti Boys inatarajiwa kuondoka nchini usiku wa kuamkia Jumatatu kwenda Shelisheli ambako itafanya mazoezi maalumu kwa ajili ya mchezo huo ambao utafanyika Septemba 18, 2016 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Hii ni mara ya pili kwa Malinzi kutimiza ahadi yake kwa wachezaji hao. Kwa mara ya kwanza aliahidi kuwapa kambi ya nje kama wangewatoa Shelisheli. Timu kweli ilikwenda Madagascar kabla ya kuivaa Afrika Kusini ‘Amajimbos’ na kuitoa na kwa sasa inakwenda Shelisheli kujipanga kwa ajili ya kuitoa Kongo-Brazzaville.
Serengeti Boys ambayo ilipiga kambi Hosteli za TFF, zilizo Karume kwa siku nne kabla ya safari hiyo na Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, Bakari Shime maarufu kama Mchawi Mweusi amesema kwamba anaamini kuwa mchezo ujao utakuwa mgumu kwa kuwa kila timu itajipanga kuvuka ili kucheza fainali hizo.
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

ANGALIA PICHA NDEGE KUBWA YA ABIRIA DUNIANI ILIYOANZA SAFARI NDEFU ZAIDI!

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

IJUE HISTORIA YA UHASIMU WA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI

LICHA YA UZURI WAKE MWANADADA ELIZABETH MICHAEL a.k.a LULU SI MALI KITU MBELE YA RAY, AMKWEPA KUOGOPA AIBU.

KWA HERI KAMANDA WETU ABBAS KANDORO

YANGA SC WAANZA KAZI AFRIKA LEO…WANAKIPIGA NA U.S.M. ALGER SAA 4:00 USIKU ALGERIA

DC MJEMA AONJA ADHA YA MAFURIKO AKIKAGUA ATHARI ZA MAFURIKO ILALA

NCHI YA URUSI NDIYO NCHI INAYOONGOZA KWA KUWA NA UBORA WA ELIMU NA VYUO DUNIANI.