NEWS ALERT: BASI LA KAMPUNI YA NEW FORCE LAPATA AJALI MBAYA MKOANI IRINGA LEO


 NEWS UPDATES.:Jumla ya watu. 12 wamepoteza Maisha na 22 wamejeruhiwa leo baada ya basi la New Force kupata ajali Eneo la Mahenge Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa barabara kuu ya Iringa- Dar es salaam..
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa,Peter Kakamba amethibitisha watu 12 kupoteza maisha katika ajali hiyo. Wanane ni wanae na wanne ni wanawake. Abiria 28 wamejeruhiwa wakiwemo madereva wa basi la lori na hali zao siyo nzuri.

Ajali hiyo imetokea majira ya saa nane alasiri ambapo basi la kampuni ya Newforce aina ya Youtong lenye namba za usajili T483CTF likitoka Tunduma kwenda Dar limegongana na lori aina ya Scania lenye namba T616DEF katika kijiji cha Mahenge,wilaya ya Kilolo Mkoa wa Iringa katika barabara kuu ya Dar - Mbeya.

Majeruhi wamelazwa hospitali ya wilaya ya Ilula.kilomita 45 kutoka Iringa mjini. 
=======  ========   ========

WATU kadhaa wanadaiwa kupoteza maisha huku wengine wengi wakijeruhiwa baada ya basi walilokuwa wakisafiria mali ya Kampuni ya NEW FORCE ONE lenye namba za usajili T483 CTF kupinduka mapema mchana wa leo katika eneo la Mahenge Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa barabara kuu ya Iringa- Morogoro, jitihada za kusafirisha majeruhi zinaendelea.
Chanzo cha ajali hiyo, inaelezwa kuwa ni Lori la mizigo lililokuwa likitokea upande wa Morogoro, kupasuka tairi ya mbele na kupoteza muelekeo uliopelekea kuligonga basi hilo na kupinduka. Globu ya Jamii inafanya jitihada za kumpata Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa kwa taarifa zaidi. tutaendelea kuwaletea taarifa kadri tutakavyozipata. Sehemu ya Basi hiyo baada ya kupata ajali.
Michuzi 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.