SAMATTA KATIKA LIGI YA UBELGIJI LEO BAADA YA VIPIGO VIWILI MFULULIZO


Na Mwandishi Wetu, GENK
BAADA ya kuanza vibaya hatua ya makundi ya Europa League kwa kufungwa mabao 3-2 na wenyeji Rapid Viena katika mchezo wa Kundi F Alhamisi Uwanja wa Allianz, Viena, Austria, mshambuliaji wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta na timu yake, KRC Genk leo wanarejea kwenye Ligi ya Ubelgiji.
Samatta na Genk yake leo watakuwa wenyeji wa Anderlecht Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Ubelgiji, wakitoka kufungwa mechi mbili mfululizo, ukiwemo wa Jumapili iliyopita walipofungwa 2-0 na Standard Liege katika Ligi ya Ubelgiji pia.
Samatta amecheza mechi mbili mfululizo bila kufunga bao, kwani Alhamisi mabao ya Genk yalifungwa na Leon Bailey yote, la kwanza dakika ya 29 na la pili dakika ya 90 kwa penalty, huku ya wenyeji, Rapid Viena yakifungwa na Stefan Schwab dakika ya 51, Joelinton Cassio Apolinario de Lira maarufu tu kama Joelinton dakika ya 59 na Omar Colley aliyejifunga dakika ya 60.
Mchezo mwingine wa kundi hilo, wenyeji Sassuolo walishinda 3-0 dhidi ya Athletic Athletic Bilbao ya Hispania Uwanja wa Citta del Tricolore, mabao ya Pol Lirola dakika ya 60, Gregoire Defrel dakika ya 75 na Matteo Politano dakika ya 82.
Tangu amejiunga na Genk Januari mwaka huu kutoka TP Mazembe ya DRC, Samatta amecheza jumla ya mechi 25 za mashindano yote, 18 msimu uliopita na saba msimu huu, akifunga mabao nane, matatu msimu huu na matano msimu uliopita.
Katika mechi hizo, ni 14 tu ndiyo alianza, 10 msimu uliopita na tatu msimu huu, wakati 11 alitokea benchi nane msimu uliopita na tatu msimu huu – na mechi tisa hakumaliza akitolewa, sita msimu uliopita na tatu msimu huu.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.