WANANCHI WENGI WAJITOKEZA ZOEZI LA USAJILI NA UTAMBUZI WA WATU MKOANI MTWARA


Zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa limeendelea mkoani Mtwara, ambapo wananchi wamejitokeza kwa wingi kujisajili, kama wakazi hawa wa Wilaya za Tandahimba na Newala walivyokutwa wakishiriki kikamilifu kujisajili.

Moja ya changamoto kubwa iliyojitokeza ni wakazi wengi hususani maeneo ya vijijini kukosa mashine za photocopy, huku baadhi wakikosa nyaraka muhimu za kuwatambulisha. Changamoto nyingine ni waombaji wengi kutokuwa na taarifa sahihi za umri wao binafsi na wazazi huku baadhi wakikosa taarifa sahihi za maeneo wanakoishi.

Hata hivyo kwa maelekezo na mafunzo yaliyotolewa na NIDA kwa maafisa wote wanaoendesha zoezi hilo changamoto nyingi zimeweza kutatuliwa kutokana na miongozo na madodoso yanayomsaidia mwombaji kutambua baadhi ya taarifa muhimu. Hata hivyo NIDA imewaomba wananchi katika maeneo mengine ambayo zoezi hili halijafanyika kuanza kujiandaa kwa kuwa na nyaraka muhimu zinazoweza kuwatambulisha mathalani; cheti cha kuzaliwa, kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi, Cheti cha Elimu ya Msingi, Sekondari au Chuo, Leseni ya Udereva, Kadi ya kupigia Kura, Pasipoti, Kadi ya Bima ya Afya, nambari ya utambulisho ya mlipa kodi (TIN) pamoja na kuwa taarifa sahihi zinazomhusu mwombaji binafsi na wazazi, majina, tarehe na miaka ya kuzaliwa. Picha na Rose Mdami ( NIDA).

Wawakilishi wa Taasisi, Mashirika na Wizara za Serikali zenye ofisi mkoani Mtwara wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mh. Mkuu wa Mkoa wa Mtwara (hayupo pichani) wakati akizindua zoezi la usajili Watumishi wa Umma mkoani humo
Baadhi wa wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Mtwara wakishiriki sherehe za uzinduzi zoezi la Usajili wa Vitambulisho vya Taifa kwa Watumishi wa Umma mkoani Mtwara 
Mmoja wa washiriki akiuliza swali wakati wa uzinduzi wa zoezi la Usajili wa watumishi wa Umma mkoani Mtwara 
Washikiri wa sherehe za uzinduzi zoezi la Usajili wa Vitambulisho vya Taifa kwa Watumishi wa Umma, mkoa wa Mtwara wakilisikiliza kwa makini maelezo ya namna ya kujaza fomu za maombi ya Vitambulisho vya Taifa 
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Hifadhi Hati Bi. Rose Mdami akifafanua jambo wakati wa uzinduzi zoezi la Usajili Watumishi wa Umma mkoa wa Mtwara; lililozinduliwa rasmi Mkuu wa Mkoa huo Bi. Halima Dendogo 
Mh. Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Halima Dendego akizungumza jambo wakati wa kuzindua zoezi la usajili wa Watumishi wa Umma mkoani Mtwara 
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Khatib Malimi Kazungu akisikiliza kwa makini majadiliano wakati wa uzinduzi wa zoezi la Usajili watumishi wa Umma mkoa wa Mtwara 
Meneja Usambazaji Vitambulisho vya Taifa Bw. George Mwandezi akitolea ufafanuzi jambo kuhusu usajili Watumishi wa Umma utakaoanza Octoba 03/2016 mkoani Mtwara 
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MATOKEO YA KIDATO CHA PILI, DARASA LA SABA YATANGAZWA ZANZIBAR

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

ZAIDI YA WANANCHI 500 KUSHIRIKI MAFUNZO YA MKIKITA YA KILIMO CHA PAPAI SALAMA

MKIKITA YATOA OFA KWA KILA HEKA YA PAPAI SH. MIL. 2 KUTANDAZA MIUNDOMBINU YA UMWAGILIAJI

WATEJA WA NSSF DAR WATIMULIWA KWA MTUTU WA BUNDUKI

PICHA:NYOKA AINA YA CHATU AUWAWA KANISANI BAADA YA KUKUTWA NYUMBANI KWA MFANYABIASHARA MAARUFU JIJINI ARUSHA AKISADIKIWA KWA IMANI ZA KISHIRIKINA

KAMISHNA MARIJANI AZINDUA CHAMA CHA WAFUGAJI MBWA TANZANIA (TCA)

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA