Assist ya Samatta imeinusuru KRC Genk na kipigo cha tano msimu huu


Baada ya watanzania kupokea good news ya nahodha wao wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Mbwana Samatta kuteuliwa katika list ya majina 30 ya wachezaji wanaowania tuzo ya mchezaji bora Afrika 2016, nyota huyo usiku wa October 15 alishuka dimbani kuisaidia timu yake ya KRC Genk kuwania point tatu ugenini dhidi ya Mouscron.
Samatta ambaye alianzia benchi na kuingia kipindi cha pili dakika ya 67 kuchukua nafasi ya mjamaica Leon Bailey, alishuhudia timu yake ya KRC Genk ikiwa nyuma kwa goli 2-1 hadi alipoingia kwenda kuongeza nguvu dakika ya 78 akafanikiwa kutoa assist na kuinusuru KRC Genk isipoteze mchezo wa tano wa Ligi Kuu Ubelgiji msimu huu.
Kufuatia matokeo hayo KRC Genk inakuwa nafasi ya 9 katika msimamo wa Ligi KuuUbelgiji, magoli ya KRC Genk yote yalifingwa na mgiriki Nikolaos Karelis dakika ya 33 baada ya kutumia vyema pasi ya Pozuelo na 78, wakati magoli ya Mouscron yalifungwaHassan Mahmoud dakika ya 3 na Valentin Viola dakika ya 42.
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

NAMAINGO YAZINDUA HEKA 7000 ZA MASHAMBA MJI KIJIJI CHA MSOLWA, MKURANGA

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

HABARI MPASUKOOO:GARI LAGONGA WATOTO KUIKWEPA BODABODA GONGO LA MBOTO

HARAMBEE YA UJENZI HOSPITALI YA MUHEZA YAVUKA MALENGO, ZAPATIKA BIL. 1.6

WAZIRI SHONZA AMJIBU DIAMOND

HABARI MPASUKOOO!!! MCHAWI ADONDOKA AKIWA UCHI KIVULE,DAR

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

DIAMOND AITWA NA NYOTA YAJAA GOMS