AZAM FC WATUA BUKOBA KUIONGEZEA MACHUNGU KAGERA SUGAR


Na Mwandishi Wetu, BUKOBA
KIKOSI cha Azam FC, kimetua salama saa 8 mchana mjini Bukoba, mkoani Kagera kikiwa na kazi moja tu ya kusaka pointi tatu muhimu katika mchezo ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) utakaofanyika kwenye Uwanja wa Kaitaba, mjini humo Ijumaa ijayo.
Wachezaji wa Azam FC pamoja na benchi la ufundi wameonekana kuwa na morali kubwa kuelekea mchezo huo, utakaofanyika katika uwanja ambao unafanana na ule wa Azam Complex unaotumiwa na matajiri hao, kutokana na vyote kuwa na nyasi bandia.
Mara baada ya kikosi hicho kuwasili mjini humo na kufikia katika Hoteli ya Smart, Kocha Mkuu wa Azam FC, Zeben Hernandez, ameweka wazi kuwa mipango yao ni kuibuka na pointi tatu hukua akieleza programu yake kwa ujumla kuelekea kipute hicho.
Hernandez amewapa mapumziko ya siku ya leo nyota wake kutokana na uchovu wa safari ndefu ya siku mbili, iliyoanzia jana alfajiri na kisha kupumzika mjini Kahama Shinyanga kabla ya leo asubuhi kuanza safari ya takribani saa sita na kuwasili mjini hapa.
Kwa mujibu wa programu ya Hernandez, kikosi hicho kitaanza kufanya mazoezi kesho kwa vipindi viwili (asubuhi na jioni) kabla ya Alhamisi kujifua kwa mara ya mwisho jioni kabla ya kupambana na Kagera Sugar ambayo imetoka kufungwa mabao 6-2 na Yanga Jumamosi iliyopita huku mabingwa hao wakiichapa JKT Ruvu bao 1-0.

0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MATOKEO YA KIDATO CHA PILI, DARASA LA SABA YATANGAZWA ZANZIBAR

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

ZAIDI YA WANANCHI 500 KUSHIRIKI MAFUNZO YA MKIKITA YA KILIMO CHA PAPAI SALAMA

MKIKITA YATOA OFA KWA KILA HEKA YA PAPAI SH. MIL. 2 KUTANDAZA MIUNDOMBINU YA UMWAGILIAJI

WATEJA WA NSSF DAR WATIMULIWA KWA MTUTU WA BUNDUKI

PICHA:NYOKA AINA YA CHATU AUWAWA KANISANI BAADA YA KUKUTWA NYUMBANI KWA MFANYABIASHARA MAARUFU JIJINI ARUSHA AKISADIKIWA KWA IMANI ZA KISHIRIKINA

KAMISHNA MARIJANI AZINDUA CHAMA CHA WAFUGAJI MBWA TANZANIA (TCA)

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA