Mwakyembe Mgeni Rasmi Maadhimisho Miaka 50 Tume ya Uchunguzi


mwakyembe-1
Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Iddi Mapuri (kushoto) akisoma taarifa yake.
mwakyembe-2
Kutoka kushoto ni Kamishna wa Haki za Binadamu na Utawala Bora, Dk. Kevin Mandopi, Mapuri, Mkurugenzi wa Utawala Bora, Hajjat Muya na Francis Nzuki.
mwakyembe-3
Wanahabari wakichukua tukio hilo.
Na Denis Mtima/Gpl
TUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kwa kushirikiana na Taasisi ya Mwalimu Nyerere zinatarajia kufanya maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa tume ya kudumu ya uchunguzi wa malalamiko ya wananchi kuhusu matumizi mabaya ya madaraka.
Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Iddi Mapuri amesema maadhimisho hayo yatafanyika Oktoba 21 mwaka huu katika Ukumbi wa Karimjee, Dar kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa saba mchana.
Amesema mgeni rasmi katika maadhimisho hayo anatarajiwa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria Dk. Harrison Mwakyembe ambapo viongozi na watu mashuhuri kutoka taasisi mbalimbali ndani na nje ya nchi watahudhuria huku maada mbalimbali zikijadiliwa juu ya utawala bora na utawala wa sheria nchini.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.