NHC YAIBUKA KIDEDEA .MAOMBI YA MBOWE HOTELS YATUPILIWA MBALI


MAHAKAMA Kuu Tanzania, Divisheni ya Ardhi, imetupilia mbali maombi ya Kampuni ya Mbowe Hotels Limited inayomikiwa na Mwenyekiti Taifa wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema), Freeman Mbowe ya kutaka kurudishwa kwenye jengo la Billicanas kwa sababu waliondolewa katika jengo la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa kufuata taratibu zote za kisheria.

Aidha, Jaji Sivangilwa Mwangesi alisema shirika hilo lilifuata taratibu zote kumwondoa mlalamikaji katika jengo hilo na kwamba inashikilia mali zake kihalali hadi atakapolipa kodi ya Sh.Bilioni 1.3 kama anavyodaiwa.

Akisoma uamuzi huo mapema jana Jaji Mwangesi baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili, mahakama yake iliamua kutupilia mbali maombi hayo yaliyofunguliwa chini ya hati ya dharula bila kulipwa gharama.

Jaji alisema madai ya mlalamikaji kwamba aliondolewa kinyume cha sheria katika jengo hilo na kampuni ya udalali isiyosajiliwa hayana mashiko kisheria mahakama inafutilia mbali kesi hiyo.

“Mahakama hii baada ya kupitia hoja za pande zote mbili imeona kwamba mlalamikiwa wa kwanza NHC alifuata taratibu zote kumtoa mlalamikaji katika jengo hilo … pia imeona kwamba kampuni ya udalali Foster Auctioneers and General Traders ilifanyakazi ya kuondoa mali zake kihali, inatupilia maombi haya bila kulipwa gharama ya kesi hii” alisema Jaji Mwangesi.

Aidha akifafanua zaidi jaji alisema pamoja na madai ya kuwepo kwa mkataba kati ya NHC na Mbowe, mkataba huo haukuwahi kutekelezwa kwa hiyo ni sawa na kwamba haupo.Upande wa mlalamikaji uliongozwa na Mawakili Peter Kibatala akisaidiana na John Mallya.

Upande wa walalamikaji uliongozwa na Mawakili Aloyce Sekule, Aliko Mwamanenge na Mariam Mungura.Wakili Mwamanenge akizungumza na Blogu ya Jamii nje ya viunga vya mahakama hiyo, alisema mlalamikaji alisema mahakama imetenda haki na kwamba mlalamikaji alidai kuwa na mkataba kati yake na NHC, lakini mahakama hiyo imeona mkataba huo haukuwahi kutekelezwa.

“Mahakama imeona dalali alifanya kazi yake kwa kufuata taratibu za kisheria na hata hizo mali zinashikiliwa na mteja kihalali hadi atakapolipa deni la Sh. Bilini 1.3 ndipo atarejeshewa mali hizo” alisema wakili Mwamanenge.

Kwa upande wake Wakili Mallya alisema wamewasilisha maombi ya kuomba nakala ya uamuzi ili waombe marejeo Mahakama ya Rufani Tanzania.

Pia, wamepeleka maombi ya kuomba chochote kisifanyike katika jengo hilo na kuhusu mali za Mbowe ni mpaka uamuzi utakapotolewa na Mahakama ya Rufani dhidi ya maombi yao ya marejeo.

Alisema Jaji katika uamuzi wake amesema mkataba kati ya NHC na Mbowe haukuwahi kutekelezwa na haupo kisheria kwa hiyo tunasubiri nakala ya uamuzi tuupitie ili tuwasilishe maombi ya marejeo mahakama ya juu” alisema Wakili Mallya.

Maombi hayo yaliyosajiliwa mahakamani hapo kwa namba 722 ya 2016 dhidi ya NHC, yalifunguliwa chini ya hati ya dharula baada ya Mbowe kuondolewa kwenye jengo hilo mapema Septemba Mosi, mwaka huu.

Katika hati ya kiapo Mbowe alidai kwamba yeye na mlalamikaji katika mgogoro huo warejee kwenye usuluhishi kwa mujibu wa mkataba wa ubia huo.

Hata hivyo, upande wa walalamikiwa ulipinga hatua hiyo kutokana na kutokuwepo kwa nyaraka hizo mahakamani hapo juu ya mwenendo wa mchakato huo wa usuluhishi, kwani walitoa ilani ya kumuhamisha Mbowe katika jengo hilo kwa kufuata sheria.

Pia ilidaiwa kuwa Mbowe katika jengo hilo ni mpangaji na hata mkataba wa ushirikiano unaodaiwa umefanyika kati yao kwa sasa hauwezi kufanyakazi kwa kuwa ulishakwisha muda wake.Katika madai ya msingi Mbowe alidai kuwa si mpangaji katika jengo hilo, bali ni mmbia ambaye anamiliki asilimia 75 katika uendeshaji wake huku NHC wakimiliki asilimia 25. 

Hoja nyingine alidai kuwa, hata kama angekuwa anadaiwa kodi kama wanavyodai NHC, kuondolewa kwake kulifanywa bila kuzingatia sheria kwani hakukuwa na amri ya mahakama inayowapa walalamikiwa nguvu ya kisheria ya kumwondoa. 

Kwa upande mwingine, Mbowe kupitia hati ya kiapo alisema hadaiwi hata senti tano na NHC kama pango la jengo la Billcanas, na kwamba amekuwa akilipa tozo zote zinazotakiwa kwa mujibu wa mkataba baina yake na shirika hilo.

Kwa mujibu wa hati ya kiapo aliyoiwasilisha mahakamani, mmiliki huyo wa Kampuni ya Mbowe Hotels Ltd alidai kwa mujibu wa mkataba wa ubia wa pande hizo mbili, anapaswa kuwalipa NHC mapato ya jengo kila mwezi.
Katika hati hiyo, Mbowe alisema hadaiwi fedha yoyote kwani amekuwa akitekeleza matakwa hayo ya kimkataba kama yalivyosainiwa mwaka 1997, huku akiambatanisha ushahidi wa risiti ya fedha ambazo amekuwa akilipa.

UPDATES...
Na Chalila Kibuda,
 Globu ya Jamii
Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Ardhi imefuta kesi iliyofunguliwa na Mbowe Hotels Ltd. dhidi ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kuwa Shirika hilo liliitoa kampuni hiyo katika jengo lake jijini Dar es salaam kwa kufuata taratibu zote na kuzishikilia mali zake kihalali.
Uamuzi huo umetolewa asubuhi hii na Jaji Sivangilwa Mwangesi, ambaye amesema madai ya Mbowe kwamba aliingia mkataba na NHC hayana mashiko na kwamba mkataba huo haukuwahi kutekelezwa.
Jengo tajwa lilikuwa na ofisi za gazeti la Tanzania daima na klabu ya Usiku ya Billicanas. Hukumu hiyo imetolewa leo na Jaji mfawidhi wa mahakama hiyo, Mhe. Sivangilwa Mwangezi ambaye amesema kuwa taratibu zote zilifuatwa kuondoa vitu katika jengo hilo.
Amesema katika hukumu hiyo hakuna mtu aliyevunjiwa haki yake ya msingi kutokana na kufuatwa kwa Sheria dhidi ya madai ya Shirika la Nyumba NHC, kwa Mbowe Hotels.
Mlalamikaji alikuwa wakidai kwamba wakati NHC inamtoa  kwenye nyumba alikuwa ndani ya Mkataba wa Ubia na NHC, lakini Jaji alikataa hilo na kusema ingawa Mkataba wa Ubia Ulikuwepo kwa kuwa haukutekelezwa ipasavyo. 

Na kwamba wakati wa NHC kumtoa kwenye nyumba Walikuwa na Mahusiano ya Mwenye Nyumba na Mpangaji, Mahusiano ambayo yako wazi kisheria juu ya Utekelezaji wake.
Wakili wa upande wa NHC, Aliko Mwamnenge amesema kutokana na hukumu hiyo Mbowe hotelS wanadaiwa sh. Bilioni 1.7 na NHC. Amesema vitu haviwezi kurudishwa mpaka pale mlalamikiwa atakapolipa deni lake kwa NHC.
Nae Wakili upande wa Mbowe Hotels, John Malya amesema wamepokea hukumu na kuomba nakala ili kuweza kuifanyia kazi. Amesema kuwa nakala wakiipata wanaweza kuamua katika kukata rufaa mapema iwezekanavyo.

Wakili wa NHC, Aliko Mwamnenge akizungumza na waandishi habari baada ya kutoka katika hukumu ya kesi iliyokuwa ikihusu maombi ya Mbowe hotels kurejea katika ofisi zake,ambapo hukumu yake imetolewa leo katika  mahakama kuu kitengo cha Ardhi,jijini Dar.
 Wakili wa Mbowe Hotels, John Malya akizungumza na waandishi wa habari juu ya hukumu iliyotelewa na Mahakama kuhusiana na maombi ya kurejea Mbowe hotels na Mali zake,  katika mahakama kuu kitengo cha ardhi leo jijini Dar es salaam.
 Mawakili wakitoka mahakamani leo mara baada ya hukumu ya kesi hiyo kutolewa. 

Mawakili wa Mbowe Hotels John Mallya (kushoto) na Peter Kibatala (kulia) wakiongea na waandishi wa habari mara tu baada ya uamuzi wa Mahakama Kuu kutoka, wakidai kwamba hawakuridhika na uamuzi wa kufutiliwa mbali kwa kesi ya mteja wao. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.