PROF. NTALIKWA AFANYA ZIARA KATIKA KITUO CHA SOMANGA FUNGU MKOANI LINDI, AWATAKA KUTUNZA MIUNDOMBINU YA GESI


Na Greyson Mwase, Lindi

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa amewataka watumishi wanaofanya kazi katika kituo cha cha kupokea gesi kutoka Madimba na Songosongo kabla ya kusafirishwa kwenda Dar es Salaam cha Somanga Fungu, kutunza mitambo na miundombinu ya mabomba ya kusafirisha gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam ili kuepuka gharama za matengenezo ya mara kwa mara.

Profesa Ntalikwa alitoa rai hiyo alipokuwa akizungumza na wafanyakazi wa kituo hicho katika ziara yake ya kukagua miundombinu ya gesi katika mikoa ya Lindi na Mtwara.

Alisema kuwa mitambo na miundombinu ya kusafirisha gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam kupitia Lindi na Pwani, inahitaji umakini wa hali ya juu katika uendeshaji wake pamoja na utunzaji ili mradi uwe na manufaa.

Alisema wananchi katika mikoa ya Lindi na Mtwara wanahitaji nishati ya umeme ya uhakika na kulitaka Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) kuhakikisha linaweka mikakati ya kuhakikisha gesi inayozalishwa inatumika ipasavyo katika uzalishaji wa umeme.

“ Kutokana na kuwepo kwa nishati ya uhakika ya gesi, Tanesco mjipange kuitumia gesi hiyo kwenye mitambo yenu na kuhakikisha kuwa baadhi ya maeneo ya Lindi yanaondokana na adha ya kukatika kwa umeme,” alisema Profesa Ntalikwa.
Mtaalam kutoka kituo cha kupokea gesi kutoka Madimba na Songosongo kabla ya kusafirishwa kwenda Dar es Salaam cha Somanga Fungu, Mhandisi Kelvin Kasian (kulia) akimwonesha Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa (kushoto) mabomba ya gesi katika kituo hicho. (hayapo pichani).
Mabomba ya kupokea gesi kutoka Madimba na Songosongo kabla ya kusafirishwa kwenda Dar es Salaam katika kituo cha Somaga Fungu kama yanavyoonekana pichani.
Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) Mhandisi Kapuulya Msomba (kushoto) akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa (katikati) katika kituo cha kupokea gesi kutoka Madimba na Songosongo kabla ya kusafirishwa kwenda Dar es Salaam cha Somanga Fungu.
Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) Mhandisi Kapuulya Msomba (kulia) akielezea matumizi ya chumba cha kuhifadhia nyaraka Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa (kushoto) katika kituo cha kupokea gesi kutoka Madimba na Songosongo kabla ya kusafirishwa kwenda Dar es Salaam cha Somanga Fungu.
Mtaalam kutoka kituo cha kupokea gesi kutoka Madimba na Songosongo kabla ya kusafirishwa kwenda Dar es Salaam cha Somanga Fungu, Mhandisi Kelvin Kasian (kulia mbele) akimwongoza Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa (kushoto mbele) kwenye ziara katika kituo hicho.
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) Dk. Shufaa Al-beity akifafanua jambo katika ziara hiyo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa akielezea mikakati ya serikali katika kuhakikisha wananchi wanapata nishati ya uhakika ya umeme katika kikao chake na wafanyakazi wa kituo cha kupokea gesi kutoka Madimba na Songosongo kabla ya kusafirishwa kwenda Dar es Salaam cha Somanga Fungu (hawapo pichani)
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika kituo cha kupokea gesi kutoka Madimba na Songosongo kabla ya kusafirishwa kwenda Dar es Salaam cha Somanga Fungu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa (wa nne kutoka kulia, waliosimama mbele) Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) Dk. Shufaa Al-beity ( wa tano kutoka kulia, waliosimama mbele) na Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) Mhandisi Kapuulya Msomba ( wa sita kutoka kulia, waliosimama mbele) wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) mara alipofanya ziara kwenye ofisi hizo.
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

ANGALIA PICHA NDEGE KUBWA YA ABIRIA DUNIANI ILIYOANZA SAFARI NDEFU ZAIDI!

LICHA YA UZURI WAKE MWANADADA ELIZABETH MICHAEL a.k.a LULU SI MALI KITU MBELE YA RAY, AMKWEPA KUOGOPA AIBU.

ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA NDANI YA CHAKE CHAKE,MKOA WA KUSINI PEMBA LEO.

IJUE HISTORIA YA UHASIMU WA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA

NCHI YA URUSI NDIYO NCHI INAYOONGOZA KWA KUWA NA UBORA WA ELIMU NA VYUO DUNIANI.

TFF YATANGAZA MAJINA YA WACHEZAJI 30 WATAKAOWANIA TUZO YA MCHEZAJI BORA MSIMU HUU