4x4

SIMBA RAHA YAICHAPA MBEYA CITY 2-0


Na Mwandishi Wetu, MBEYA
SIMBA SC imejiweka sawa kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mbeya City jioni ya leo Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Shukrani kwa wafungaji wa mabao hayo Ibrahim Hajib Migomba na Shizza Ramadhan Kichuya, wote kipindi cha kwanza na sasa Wekundu wa Msimbazi wanafikisha pointi 20 baada ya mechi nane.
Hajib alianza kuifungia Simba SC dakika ya sita baada ya shuti lake la mpira wa adhabu kufuatianKichuya kuangushwa kumshinda mlinda mlango kutoka Malawi, Owen Chioma. mpira wa faulo ukapita moja kwa moja wavuni, faulo ilitokana na Kichuya kuangushwa
Kichuya mwenyewe akafunga bao la pili dakika ya 37 baada ya kuambaa na mpira wingi ya kushoto na kwenda kumtungua Chioma.
Simba SC ingemaliza kipindi cha kwanza ina mabao zaidi ya mawili kama Muivory Coast, Frederick Blagnom kupoteza nafasi za wazki kikiwemo penalty dakika ya 15 kufuatia yeye mwenyewe kuangushwa, lakini mkwaju wake ulipanguliwa na kiopa Chioma.
Kikosi cha Simba kilikuwa; Vincent Agban, Janvier Bukungu, Mohammed Hussein 'Tshabalala', Method Mwanjali, Novart Lufunga, Mkude Jonas, Muzamil Yassin, Kazimoto Mwinyi Kichuya, Shiza Kichuya, Frederick Blagnon na Ibrahim Hajib.
Mbeya City; Owen Chaima, John Kabanda, Michael Kerenge, Tumba Swedi, Rajab Zahir, Sankhani M, Joseph Mahundi, Kennu Ally, O Ramadhani, Raphael Daudi na Ditram Nchimbi.
Post a Comment