FORBES LIST: Mastaa wenye miaka chini ya 30 na wanalipwa pesa nyingi zaidi

Baada ya mwezi September kutolewa list ya Hip Hop Cash Kings, Jarida linalofatilia maisha ya watu maarufu duniani FORBES, limetaja list ya mastaa 30 wenye miaka chini ya 30 na wanalipwa pesa nyingi zaidi duniani. List hii inajumuisha mastaa wa (Michezo, Music, Uigizaji na wengineo).
Mwimbaji Taylor Swift, ambaye haweki kabisa vionjo vya muziki wa hip-hop na r’n’b,ameshika nafasi ya #1. Star huyu mwenye miaka 26 ametajwa kuingiza zaidi ya Dola za Marekani Milioni 170 ndani ya mwaka mmoja na kiasi kikubwa kikitokana na mauzo ya albam yake iitwayo 1989 pamoja na ziara ya muziki.
Star mdogo kuliko wote kwenye list hiyo Justin Bieber, mwenye miaka 22 ameshika nafasi ya #6 baada ya kuingiza kiasi cha Dola za Marekani Milioni 56. Rapa kutoka YMCMB Drake naye ametajwa kwenye list ameshika nafasi ya #17 akiwa na umeingiza Dola za Marekani Milioni0 38 kwenye akaunti zake.
Pia wamo mastaa wa michezo, kama Kyrie Irving mwenye miaka 24 ameshika nafasi ya #30 akiwa ameingiza dola milioni 28.5, mwanariadha Usain Bolt yuko kwenye nafasi ya #27 akiwa na dola milioni 32.5, James Harden ameshika nafasi ya #26 akiwa na dola miliini 33 na Cam Newton kwenye nafasi ya #10 anaingiza milioni 53 akiwa amefungamana na The Weeknd).
Nimekuwekea Top 5 ya mastaa walioingiza pesa nyingi mwaka 2016 wakiwa chini ya miaka 30.
  1. Taylor Swift (26) – Dola Milioni 170 
  2. One Direction – Dola Milioni 110
  3. Lionel Messi (29) – Dola Milioni 81.5
  4. Adele (28) – Dola Milioni 80.5 
  5. Rihanna (28) – Dola Milioni 75 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.