MAGHEMBE:SEKTA YA UTALII YAKUA KWA KASI HUKU MAPATO YAKIFIKIA DOLA BIL.2




Baadhi ya wahitimu katika mahafali ya sita ya chuo cha utalii na hotel Njuweni,Kibaha mkoani Pwani,wakisoma risala kwa mgeni rasmi kwenye mahafali hayo,waziri wa maliasili na utalii prof,Jumanne Maghembe



Mlezi wa chuo cha utalii na hotel Njuweni,Kibaha,Yusuph Mfinanga akizungumza jambo katika mahafali ya sita ya chuo hicho.

Waziri wa maliasili na utalii,prof Jumanne Maghembe ,akionekana akizungumza katika mahafali ya sita ya chuo cha utalii na hotel Njuweni,Kibaha mkoani Pwani(Picha zote na Mwamvua Mwinyi)

Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
WAZIRI wa maliasili na utalii,prof.Jumanne Maghembe, amesema sekta ya utalii kwasasa inachangia dola bil.2 katika pato la Taifa kwa mwaka kutoka dola mil.800 iliyokuwa ikichangia kipindi cha nyuma.
Aidha amesema serikali imeajiri watanzania 500,000 moja kwa moja katika sekta hiyo ambapo wengine mil.moja wamejiajiri wenyewe hali iliyosababisha kupunguza idadi  kubwa ya wahitimu kusota wakitafuta ajira hiyo.
Katika hatua nyingine,prof.Maghembe amewataka wahitimu wa masuala ya utalii nchini kutangaza vivutio vya  Tanzania na kutoa huduma bora wakati wanapopata ajira ili kuhamasisha watalii wa nje na kuongeza pato la taifa.

Waziri huyo aliyasema hayo ,kwenye mahafali ya sita ya chuo cha hotel na utalii cha Njuweni kilichopo mjini Kibaha,wakati alipokuwa mgeni rasmi.

Alieleza kuwa sekta hiyo inakua kwa kasi kimapato na kuongeza idadi ya watalii kila siku kwa asilimia 100 ukilinganisha na miaka kumi iliyopita.
Prof.Maghembe alisema ni matumaini yake miaka mitatu ijayo mapato yataongezeka mara tatu zaidi ya ilivyo sasa.
Aliwataka wahitimu kuacha kujibweteka na elimu waliyoipata bali waendelee kujifunza lugha mbalimbali na mafunzo ya fani hiyo ili kuongeza taaluma zao.
“Kama hamtofanya hivyo mtapunguza idadi ya watalii ,msibweteke tumieni elimu yenu mliyoipata ili kuvutia watalii waendelee kuja Tanzania na kupeleka sifa kwenye nchi zao kutokana na ukarimu ,mapokezi na utoaji wenu huduma" alisema prof.Maghembe.
Nae mkurugenzi wa chuo hicho Saidi Mfinanga,alisema njuweni ni kati ya vyuo vya mwanzo katika sekta ya hotel na utalii nchini na imechangia kwa kiwango kikubwa sekta hiyo.

Alielezea kwamba kuanzia mwaka 2000 hadi 2015 chuo hicho kimetoa wahitimu 6,832 ambao wameingia katika soko la ajira nchini, katika upande wa hotel yaani hotel management  na uongozaji watalii.
Saidi alisema mapema mwaka huu chuo kilipata nafasi ya kualikwa katika mashindano ya 14 ya mapishi duniani,yaliyoitwa(14th international Istanbul gastronomy festival 2016)yaliyofanyika katika jiji la instabul nchini Uturuki huku kati nchi 36 zilizoshiriki ilishinda nafasi ya pili.
Aliwaomba wazazi kuchangamkia fursa ya elimu wanayotoa kwa kupeleka watoto wao waliomaliza kidato cha nne na cha sita na kukosa nafasi ya kuendelea na masomo.
Nae mlezi wa chuo hicho Yusuph Mfinanga alisema chuo hicho kinakabiliwa na changamoto ya upungufu wa vifaa vya kisasa vya kuendesha masomo ya TEHAMA .
Alisema ili kuendana na ulimwengu wa leo TEHAMA ni mhimili mkubwa katika kila eneo la kiutendaji ambapo chuo kina mpango wa kuendesha kozi ndefu hadi kufikia diploma kwenye ngazi hiyo.
Mfinanga alimuomba waziri huyo kuwasaidia kupata msaada wa vifaa vipya kwa masomo hayo kwani chuo kimedhamiria kutoa mafunzo kwa mtandao kwa kila mwanafunzi kutumia komputa yake .
Mkuu wa chuo hicho Nditi Rashid alisema chuo cha njuweni kilianzishwa January 2000 kwa malengo ya kutoa elimu ya utalii na hotel ili kuboresha huduma katika sekta hiyo nchini.

Alisema chuo hicho kwasasa ni kikubwa ,lakini kilipo ni sehemu finyu kwa mahitaji ya sasa hivyo kuna kilasababu ya kuongezwa ukubwa ili kukidhi mahitaji.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.