MAGUFULI: VYOMBO VYA HABARI SIMAMIENI KUJENGA MAADILI NA UTAMADUNI WA MTANZANIA.







Na Daudi Manongi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.John Pombe Magufuli ametoa wito kwa vyombo vya Habari nchini kuwa mbele katika kusimamia Maadili na kuutangaza Utamaduni wa  Mtanzania.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo Ikulu Jijini Dar es Salaam wakati wa Mahojiano ya mwaka na waandishi wa habari kwa mara ya kwanza tangu aingie madaraka.

“Jukumu la kulinda Utamaduni na Maadili ya mtanzania ni la kila mzalendo, mtanzania, mzazi  na Wizara husika ipo kwa ajili ya kusimamia jambo hili na vyombo vya habari mnatakiwa kuwa mstari wa mbele kulisimamia kwa kuanzia katika vyombo vyenu vya Habari kutokana na kile mnachoonyesha”Alisema Rais Magufuli.

Aidha Rais Magufuli amevitaka vyombo vya Habari kuwa wazalendo katika kutengeneza vipindi vyenye mahadhi ya kitanzania ili kuisaidia jamii kukua katika utamaduni wetu na kusaidia kujenga maadili yaliyo bora.

Mbali na hayo Rais Magufuli amezungumzia mafanikio mbalimbali yaliyopatikana katika kipindi chake cha mwaka mmoja toka aingie madarakani ikiwemo kuongezeka kwa mapato kutoka bilioni 800 mpaka makusanyo ya shilingi trilioni 1.5 kwa mwezi.

Pia amesema kuwa Bajeti ya mwaka 2016 ya trilioni 29.5 iliyotenga asilimia 40 kwenye miradi ya maendeleo imekuwa yenye mageuzi makubwa ukilinganisha na bajeti ya miradi hapo nyuma mabayo ilikuwa asilimia 26 tu.

Pamoja na hayo Rais magufuli amesema kuwa Serikali imeagiza ndege nyingine mbili zinategemewa kufika nchini mwanzoni mwa mwaka 2018 ili kuboresha sekta ya utalii nchini.

Akizungumzia uundwaji wa serikali amesema mategemeo yake katika serikali aliyoiunda imefanikiwa kwa kuwa Baraza aliloliunda la watu wachache limekuwa la mafanikio makubwa na hili limetokana na ushirikiano mkubwa wa mawaziri wake.


Rais Magufuli amevitaka vyombo vya habari nchini kubadili mtazamo wao katika uandishi wao wa habari na kuandika habari ambazo zina maslahi kwa Taifa na kuwahakikishia waandishi wa habari kushirikiana nao kwa kuwa anatambua kazi nzuri wanayoifanya.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.