SIMBA KAPAKATWA NA PRISONS 2-1 MBEYA

Na David Nyembe, MBEYA
NGUVU ya soda? Hilo ndilo swali unaloweza kujiuliza baada ya Simba SC kupoteza mchezo wa pili mfululizo leo kufuatia mwanzo mzuri katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Simba iliyoanza vyema Ligi Kuu na kucheza mechi 13 mfululizo bila kupoteza, ikishinda 11 na sare mbili – ilipoteza mechi ya kwanza Jumapili kwa kufungwa na African Lyon 1-0 Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Na leo imepoteza mchezo wa pili kwa kufungwa 2-1 na wenyeji Prisons Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Katika mchezo wa leo, shujaa wa Prisons alikuwa ni mchezaji wa zamani Rhino Rangers ya Tabora, Victor Hangaya aliyefunga mabao yote mawili, baada ya Jamal Simba Mnyate kutangulia kuifungia Simba.
Kocha Mcameroon, Joseph Marius Omog hana raha baada ya Simba kupoteza mechi ya pili mfululizo Ligi Kuu leo

Mnyate alifunga dakika ya 43 akimalizia kwa kichwa krosi nzuri ya winga Shizza Ramadhani Kichuya kutoka upande wa kushoto.
Simba ikaenda kupumzika inaongoza 1-0 na dakika mbili tu baada ya kuanza kipindi cha pili Hangaya akaisawazishia Prisons akimalizia krosi ya Salum Bosco kabla ya kufunga la pili dakika ya 64 akimalizia kwa kichwa mpira wa adhabu wa Mohammed Samatta.
Simba SC ilipambana kusaka bao la kusawazisha, lakini bahati mbaya wakaishia kukosa mabao ya wazi.
Nafasi nzuri zaidi alipoteza Kichuya dakika ya 83 baada ya kupiga shuti kali na mpira ukatoka nje pembeni sentimita chache na dakika ya 85 akapiga kona maridadi iliyokwenda nje kidogo ya lango.
Kwa matokeo hayo, Simba SC inamaliza mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu na pointi zake 35 baada ya kucheza mechi 15, wakifuatiwa na mabingwa watetezi, Yanga wenye pointi 30 ambao leo wanacheza mechi yao ya mwisho ya mzunguko wa kwanza na Ruvu Shooting Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. 
Kikosi cha Prisons kilikuwa; Andrew Ntala, Benjamin Asukile, Salum Kimenya, Leonsi Mutalemwa, James Mwasote, Njinjai Kazungu, Jumanne Elfadhil, Lambarti Sabiyanka, Mohemmed Samatta, Victor Hangaya na Salum Bosco.
Simba SC; Vincent Agban, Hamadi Juma, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Novaty Lufunga, Method Mwanjali, Jonas Mkude/Mussa Ndusha dk82, Shizza Kichuya, Muzamil Yassin, Laudit Mavugo, Mwinyi Kazimoto/Ibrahim Hajib dk69 na Jamal Mnyate.

0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MATOKEO YA KIDATO CHA PILI, DARASA LA SABA YATANGAZWA ZANZIBAR

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

ZAIDI YA WANANCHI 500 KUSHIRIKI MAFUNZO YA MKIKITA YA KILIMO CHA PAPAI SALAMA

MKIKITA YATOA OFA KWA KILA HEKA YA PAPAI SH. MIL. 2 KUTANDAZA MIUNDOMBINU YA UMWAGILIAJI

WATEJA WA NSSF DAR WATIMULIWA KWA MTUTU WA BUNDUKI

DIAMOND AITWA NA NYOTA YAJAA GOMS

KAMISHNA MARIJANI AZINDUA CHAMA CHA WAFUGAJI MBWA TANZANIA (TCA)

PICHA:NYOKA AINA YA CHATU AUWAWA KANISANI BAADA YA KUKUTWA NYUMBANI KWA MFANYABIASHARA MAARUFU JIJINI ARUSHA AKISADIKIWA KWA IMANI ZA KISHIRIKINA