SAMATTA AKIPIGA DAKIKA ZOTE 90, LAKINI GENK YAFA 6-0 UGENINI


Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta amecheza dakika zote 90 leo, lakini timu yake KRC Genk imefungwa mabao 6-0 na KV Oostende katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji.
Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Versluys Arena mjini Oostende, Genk ilicheza pungufu baada ya mshambuliaji wake Mjamaica, Leon kuonyeshwa kadi ya pili ya njano na kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 68.
Mabao ya Oostende yalifungwa na kiungo Muargentina Franck Berrier dakika ya 19, beki Mcroatia, Antonio Milic dakika ya 29, mshambuliaji Mzimbabwe, Knowledge Musona dakika ya 56, mshambuliaji Landry Nany Dimata kutoka DRC mawili dakika ya 71 na 86 na mshambuliaji Muivory Coast, Gohi Bi Zoro Cyriac dakika ya 83.
Huu ulikuwa mchezo wa kwanza Samatta kuanza baada ya mechi tatu mfululizo za kutokea benchi tangu alipoanza mara ya mwisho Novemba 3 dhidi ya Athletic Bilbao kwenye Europa League.
Mshambuliaji Mgiriki, Nicolous Karelis aliyekuwa anaanza mechi zilizopita mbele ya Samatta leo alikuwa ben chi muda wote.
Makali ya Samatta yalianza kupungua baada ya kuumia kwenye mchezo wa Europa League dhidi ya Rapid Wien ya Austria Septemba 15, mwaka huu Genk ikishinda 3-2 Uwnja wa Laminus Arena.
Na siku hiyo, Samatta alishindwa kuendelea na mchezo baada ya kuumia na kutoka dakika ya 78, nafasi yake ikichukuliwa na Mbelgiji Karelis. 
Samatta alikaa nje kwa wiki tatu na tangu hapo hata baada ya kurejea hakupata nafasi ya kuanza kutokana Karelis kufanya vizuri kabla ya kurejea leo.
Leo Samatta amecheza mechi ya 35 tangu amejiunga na Genk Januari mwaka huu kutoka TP Mazembe ya DRC, 18 msimu uliopita na 15 msimu huu, akifunga mabao nane, matatu msimu huu na matano msimu uliopita.
Katika mechi hizo, ni 18 tu ndiyo alianza, 10 msimu uliopita na sita msimu huu, wakati 16 alitokea benchi nane msimu uliopita na 13 msimu huu – na mechi 10 hakumaliza akitolewa, sita msimu uliopita na nne msimu huu.
Kikosi cha KV Oostende leo kilikuwa; Ovono, Marusic/Godeau dk73, Rozehnal, Milic, Vandendriessche, Jonckheere/Cyriac dk81, Siani, Berrier, Musona/El Ghanassy dk69 Canesin na Dimata.
KRC Genk: Bizot, Wouters, Colley, Brabec, Castagne, Ndidi, Heynen/Susic dk45 Pozuelo/Kumordzi dk77, Bailey, Samatta na Buffalo/Trossard dk66.

0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

MAMEYA WA TEMEKE, UBUNGO WATWANGANA UCHAGUZI WA NAIBU MEYA DAR

IJUE HISTORIA YA UHASIMU WA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI

LICHA YA UZURI WAKE MWANADADA ELIZABETH MICHAEL a.k.a LULU SI MALI KITU MBELE YA RAY, AMKWEPA KUOGOPA AIBU.

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

MATOKEO YA KIDATO CHA PILI, DARASA LA SABA YATANGAZWA ZANZIBAR

PICHA:NYOKA AINA YA CHATU AUWAWA KANISANI BAADA YA KUKUTWA NYUMBANI KWA MFANYABIASHARA MAARUFU JIJINI ARUSHA AKISADIKIWA KWA IMANI ZA KISHIRIKINA