Binti aliyefanyiwa upasuaji wa moyo na kupona na asherehekea na Wagonjwa wa Moyo waliolazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)


Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akipokea zawadi za pampers ambazo zitatumika kwa watoto waliolazwa kutoka kwa Mary Mabano ambaye mwaka 2008 alifanyiwa upasuaji na madaktari wa Taasisi hiyo na kuwekewa Valve moja ambayo inamsaidia kupitisha damu vizuri baada ya upasuaji huo amepona na amejaliwa kupata mtoto mmoja. Siku ya jana tarehe 28/12/2016 Mary alikuwa anatimiza umri wa miaka 23 na aliamua kusherehekea siku hiyo na wagonjwa wa moyo.
Mary Mabano akimlisha keki mgonjwa wa Moyo Nasra Hamis ambaye amefanyiwa upasuaji na kuwekewa Valve ambayo inamsaidia kupitisha damu vizuri katika moyo wake.
Madaktari Bingwa wa Moyo, Wauguzi , wagonjwa wa Moyo, ndugu, jamaa na marafiki wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa sherehe ya kuzaliwa kwa Mary Mabano ambaye aliyesherehea siku hiyo na wagonjwa wa Moyo waliolazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI). Wa tano kutoka kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Prof. Mohamed Janabi.

Mary Mabano akimkabidhi Afisa Muuguzi Msaidizi ambaye pia ni msimamizi wa wodi namba tatu (3) iliyoko Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Rogers Kibula zawadi ya sabuni ya unga ya kufulia ambayo itatumika kwa ajili ya usafi wakati wa sherehe yake ya kutimiza miaka 23 iliyofanyia jana katika Taasisi hiyo. Mary alisherehekea siku yake ya kuzaliwa na wagonjwa wa Moyo kwa kuwa hata yeye mwaka 2008 alifanyiwa upasuaji wa moyo na kuwekewa Valve moja ambayo inamsaidia kupitisha damu vizuri baada ya upasuaji huo amepona na amejaliwa kupata mtoto mmoja.
Mary Mabano akiwa katika picha ya pamoja na Daktari Bingwa wa Moyo ambaye ndiye daktari anaendelea kumtibu Tulizo Shemu Sanga, baba yake mzazi Mzee Fabian Mabano ambaye amembeba mjukuu wake mtoto wa Mary aitwaye Faraj Khalid.
Mary Mabano akimlisha keki Mtoto Jumanne Mndeme ambaye amelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya matibabu ya moyo.
Picha ya keki ya Siku ya kuzaliwa Mary Mabano.
Mary Mabano akimlisha keki Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo Tulizo Shemu Sanga ambaye ndiye daktari anaendelea kumtibu Mary. Mwaka 2008 Mary alifanyiwa upasuaji wa moyo na kuwekewa Valve moja kwa kuwa Valve yake ya kuzaliwa nayo ilikuwa na tatizo la kutokupitisha damu vizuri.
Mary Mabano akikata keki wakati wa kusherehekea siku yake ya kuzaliwa huku Madaktari Bingwa wa moyo, wauguzi, ndugu na jamaa wakishuhudia. Picha na Anna Nkinda - JKCI

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.