KOTEI ASAINI MWAKA MMOJA SIMBA, ANGBAN, NDUSHA WATUPIWA VIRAGO


Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
KIUNGO Mghana, James Kotei amesaini mkataba wa mwaka mmoja kujiunga na Simba, huku kiungo Mussa Ndusha kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) akiachwa.
Kamati ya Usajili ya Simba ilikuwa ina kikao jana kukamilisha zoezi la marekebisho ya usajili kabla ya kufungwa kwa dirisha dogo na katika kikao hicho ilikubaliana pia kumsajili mshambuliaji Mtanzania Juma Luizo aliyekuwa Zesco United ya Zambia.
Aidha, Simba imempandisha Nahodha wa kikosi cha U-20 Moses Kitundu hayo yakiwa mapendekezo ya kocha Mcameroon, Joseph Marius Omog.
James Kotei (kushoto) amesaini mkataba wa mwaka mmoja kujiunga na Simba

Kitundu aling’ara katika michuano ya Ligi ya Vijana chini ya umri wa miaka 20 iliyomalizika Jumapili Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam kwa Simba kuchukua ubingwa ikiifunga Azam kwa penalti 5-3 baada ya sare ya 2-2 ndani ya dakika 120.
Pamoja na hayo, Simba imemsajili mshambuliaji Pastory Athanas kutoka Stand United ya Shinyanga.
Mbali na Ndusha anayetolewa kwa mkopo kwa kuwa bado ana mkataba na klabu, Simba pia inamuacha kipa Muivory Coast Vincent Angban baada ya kusajili kipa Mghana, Daniel Agyei. 
Waghana Agyei na Kotei wanaungana na wachezaji wengine watano wa kigeni wa Simba kukamilisha idadi ya wachezaji saba kwa mujibgu wa kanuni za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Hao ni mabeki Janvier Bokungu kutoka DRC, Method Mwanjali (Zimbabwe), Juuko Murshid (Uganda) na washambuliaji Laudit Mavugo (Burundi) na Frederick Blagnon (Ivory Coast). 
Sasa Simba inashughulikia uhamisho wa wachezaji wapya ili wawahi kucheza mechi ya kwanza mzunguko wa pili wa Ligi Kuu dhidi ya Ndanda FC mjini Mtwara Jumapili wiki hii.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.