MASAUNI AFANYA ZIARA NIDA ZANZIBAR, ATEMBELEA WAGONJWA NA KUFANYA USAFI HOSPITALI YA MNAZI MMOJA


 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akimkabidhi Kitambulisho cha Taifa cha Wageni, Leonie Schollmeyer (kulia), wakati kiongozi huyo alipofanya ziara ya kikazi katika Ofisi za Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Zanzibar leo. Masauni licha ya kupewa elimu kuhusiana na utendaji wa kazi wa ofisi hiyo, pia alizungumza na watumishi wa Mamlaka hiyo na kuwataka kufanya kazi kwa weledi kwa kuwahudumia wananchi ili kuiletea mamlaka hiyo mafanikio zaidi.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akifanya usafi na wanachama wa Baraza la Vijana Shehia ya Miembeni katika Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar. Masauni alialikwa na Baraza hilo kushiriki kufanya usafi nao na baadaye aliwatembelea wagonjwa wa hospitali hiyo akiwa na Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi, Mgeni Hassan Juma (hayupo pichani) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Mjini, Marina Joel Thomas (hayupo pichani).  
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na Watumishi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Zanzibar wakati kiongozi huyo alipofanya ziara ya kikazi ya kujifunza shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka hiyo. Masauni licha ya kupewa elimu kuhusiana na utendaji wa kazi wa ofisi hiyo, pia alizungumza na watumishi wa Mamlaka hiyo na kuwataka kufanya kazi kwa weledi kwa kuwahudumia wananchi ili kuiletea mamlaka hiyo mafanikio zaidi. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo, Zanzibar, Hassan Haji Hassan.
 Spika wa Baraza la Wawakilishi, Mgeni Hassan Juma (kushoto), Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa kofia) wakimsikiliza Nesi Msaidizi Mkuu wa Wodi ya Upasuaji wa Uti wa Mgongo na Kichwa katika Hopsitali ya Mnazi Mmoja, Hadia Mmadi, wakati alipokuwa anawafafanulia kuhusu wagonjwa wanavyopasuliwa. Viongozi hao walifanya ziara katika eneo hilo, mara baada ya kufanya usafi mazingira mbalimbali ya hospitalini hapo.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (watatu kushoto mstari wa mbele), Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Zanzibar, Hassan Haji Hassan (watatu kulia)  wakiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Mamlaka hiyo, mara baada ya Masauni kumaliza ziara yake ya kikazi kuitembelea Mamlaka hiyo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa kofia) akiwa katika picha ya pamoja na Wanachama wa Baraza la Vijana Shehia ya Miembeni, Kikwajuni, Zanzibar, mara baada ya kumaliza kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya Hospitali ya Mnazi Mmoja. Vijana hao walimwalika Mbunge wao ili wajumuike naye katika kuweka safi zaidi mazingira ya Hospitali hiyo.  Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

NAMAINGO YAZINDUA HEKA 7000 ZA MASHAMBA MJI KIJIJI CHA MSOLWA, MKURANGA

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

DIAMOND AITWA NA NYOTA YAJAA GOMS

HABARI MPASUKOOO:GARI LAGONGA WATOTO KUIKWEPA BODABODA GONGO LA MBOTO

HARAMBEE YA UJENZI HOSPITALI YA MUHEZA YAVUKA MALENGO, ZAPATIKA BIL. 1.6

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

PICHA:NYOKA AINA YA CHATU AUWAWA KANISANI BAADA YA KUKUTWA NYUMBANI KWA MFANYABIASHARA MAARUFU JIJINI ARUSHA AKISADIKIWA KWA IMANI ZA KISHIRIKINA

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA