Marais wa Marekani wakitoka White House huenda wapi?



Barack Obama wavingHaki miliki ya pichaREUTERS
Barack Obama ameondoka madarakani baada ya kuongoza Marekani mwa miaka minane, na akampisha Donald Trump.
Obama alifanyia utani maisha yake ya baada ya kustaafu na kusema angependa kufanyia kazi Spotify, lakini anataka kuendelea kujihusisha na siasa.
Lakini ingawa anatarajiwa kuandika kitabu, na kuhojiwa mara kwa mara kwenye runinga, hajaficha mengi kuhusu anayoyapanga.
Lakini labda anaweza kupata mawazi kutoka kwa baadhi ya marais 42 waliomtangulia?

John Adams (1797-1801)

John AdamsHaki miliki ya pichaASHER B DURAND
Baada ya kuongoza kwa miaka minne kama rais wa Marekani, John Adams alistaafu na kuishi maisha ya kimya na mkewe Abigail.
Aliishi kwa miaka mingine 25 akiwa amezungukwa na jamaa zake wa karibu.
Alitumia muda wake mwingi kuandika.
Alifariki siku moja na Thomas Jefferson, rais wa tatu wa Marekani mnamo 4 Julai 1826, miaka 50 baada ya Marekani kujitangazia uhuru wake.

James Madison (1809-1817)

James MadisonHaki miliki ya pichaJOHN VANDERLYN
James Madison alimiliki shamba kubwa la kilimo na baada ya kustaafu, alirejelea kazi yake shambani, ambapo alikuwa anamiliki watumwa.
Alikuwa mwanachama wa shirika la American Colonization Society, lililotaka kuwarejesha watumwa Afrika.

William Henry Harrison (1841)

William Henry HarrisonHaki miliki ya pichaALBERT GALLATIN HOIT
Rais huyu wa tisa wa Marekani ndiye aliyehudumu kwa muda mfupi zaidi na ndiye wa kwanza kufariki akiwa madarakani nchini humo.
Alifariki siku 32 baada ya kuapishwa, kutokana na homa kichomi (nimonia).
Taarifa nyingi hudai alipata homa hiyo alipokuwa anatoa hotuba yake ndefu sana kukiwa na hali mbaya ya hewa. Hakuna ushahidi wa kuthibitisha hilo.
Grover Cleveland (1885-1889 na 1893-1897)
Grover ClevelandHaki miliki ya pichaUS NATIONAL ARCHIVES AND RECORDS ADMINISTRATION
Grover Cleveland ndiye mtu pekee aliyeongoza muhula mmoja kama rais Marekani, akaondoka na kisha kurejea baadaye. (Hii ndiyo sababu ingawa Barack Obama ni rais wa 44 wa Marekani, ni marais 42 waliokuwa nyuma yake na si 43).

Theodore Roosevelt (1901-1909)

Theodore RooseveltHaki miliki ya pichaPACH BROTHERS
Theodore Roosevelt alijaribu kuwania urais muhula wa tatu 1912 lakini akashindwa na Woodrow Wilson (kabla ya 1951 hakukuwa na kikomo katika mihula ya rais).
Baadaye, alimchukua mwanawe Kermit na wakaenda kutalii Mto wa Doubt nchini Brazil.
Aliugua malaria na jeraha mguuni katika mazingira magumu Brazil, na nusura afariki.

Richard Nixon (1969-1974)

Richard Nixon
Kashfa ya Watergate alimlazimisha Richard Nixon wa Republican kujiuzulu.
Utawala wake ulijaribu kuficha habari baada ya wizi katika makao makuu ya Kongamano la Kitaifa la chama cha Democratic kubaini kwamba wapinzani wake walikuwa wananakiliwa mazungumzo yao kisiri.
Nixon alikabiliwa na matatizo ya kiafya na kifedha wakati huo.
Baadaye, aliuza kitabu kuhusu maisha yake, na pia akalipwa kufanya mahojiano. Mwishowe, alirejea katika siasa za dunia.

Jimmy Carter (1977-1981)

Jimmy Carter
Huwa anatazamwa kama mfano mwema kuhusu yale marais wa Marekani wanafaa kufanya baada ya kuondoka madarakani.
Jimmy Carter, ambaye sera yake ya kigeni haikuingia doa, amekuwa akifanya katika kampeni za kusaidia jamii, kufanya diplomasia ya kimataifa na kuandika vitabu kadha.
Mwaka 2002, alitunukiwa Tuzo ya Amani ya Nobel.
Ana miaka 92 sasa lakini bado anajihusisha na miradi ya hisani kama vile ujenzi wa makao kwa watu wasiojiweza.
Alikuwa rais wa zamani wa kwanza kuthibitisha angehudhuria sherehe ya kuapishwa kwa Trump.
Viashiria kuhusu Barack Obama (2009-2017)
Barack na Michelle Obama walitangaza kwamba baada ya kupumzika wka muda, watafungua "kituo kuhusu uongozi" mjini Chicago.
Marais wengi ambao hustaafu sana hufungua maktaba katika majimbo yao.
Lakini Obama anasema maktaba yake itakuwa "kituo kuhusu uongozi" na kitapokea maoni kutoka kwa raia ambao viongozi chipukizi na mashirika yanafaa kuwa yanaunga mkono.

Mada zinazohusiana

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.