Guardiola: Man City sharti tufunge mabao mengi Monaco


Pep GuardiolaHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionSergio Aguero sasa amefunga mabao mawili na zaidi katika mechi saba msimu huu
Manchester City "wataondolewa" kwenye michuano ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya iwapo hawatafunga katika mechi ya marudiano hatua ya 16 bora dhidi ya Monaco, meneja wao Pep Guardiola amesema.
City walitoka nyuma mara mbili na hatimaye wakafanikiwa kuwalaza viongozi hao wa ligi ya Ufaransa 5-3 mechi ya kusisimua iliyochezewa uwanja wa Etihad.
Mechi ya marudiano itachezwa 15 Machi.
"Tutasafiri Monaco na kufunga mabao mengi kadiri iwezekanavyo," Guardiola alisema baadaye.
"Hilo ndilo lengo langu. Ni vigumu kwetu kusonga tusipofunga bao."
Monaco waliongoza 2-1 na 3-2 kabla ya City kujikwamua na kupata ushindi.
Mechi hiyo inaongoza kwa kufungwa mabao mengi miongoni mwa mechi za mkondo wa kwanza hatua ya muondoano katika miaka 25 ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Guardiola anatarajia mechi iwe wazi sana klabu hizo zitaapokutana tena.
Anahisi hiyo ndiyo njia bora zaidi ya kukabiliana na mashambulio makali ya Monaco ambao wamefunga mabao 76 mechi 26 za ligi Ufaransa msimu huu.
Willy CaballeroHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionManchester City wamekomboa penalti zote tano zilizopigwa karibuni zaidi dhidi yao Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya (mbili na Caballero, tatu na Joe Hart)
"Wanacheza kwa njia hiyo - watashambulia na kushambulia," alisema Guardiola.
"Tutahitaji kujilinda zaidi lakini tutapata nafasi. Nina uhakika kuhusu hilo.
"Je, nina furaha timu yangu ikifungua mchezo? Ndio. Sana."
Rekodi ya Pep Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya
MsimuKlabuHatua Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya
2008-09BarcelonaFainali (wakawalaza Man Utd 2-0)
2009-10BarcelonaNusufainali (3-2, wakashindwa na Inter)
2010-11BarcelonaFainali (wakalaza Man Utd 3-1)
2011-12BarcelonaNusu fainali (3-2, wakalazwa na Chelsea)
2013-14Bayern MunichNusu fainali (5-0 , wakalazwa na Atletico Madrid)
2014-15Bayern MunichNusu fainali (5-3 , wakalazwa na Barcelona)
2015-16Bayern MunichNusu fainali (2-2 sare na Atletico. Atletico wakasonga kwa magoli ya ugenini)

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.