MWANAMKE ALIYETELEKEZWA NA MMEWE AFANYE NINI KISHERIA.




Image result for MAMA AMETELEKEZWA
NA  BASHIR  YAKUB -

Kutelekezwa  ni  pamoja  na  kunyimwa  huduma  za  muhimu  ambazo  kama  mke  alistahili  kupata. Huduma  muhimu  ni  kama  chakula, mavazi  ,  makazi,  matibabu, hela  ya  kujikimu  kwa  matumizi  ya  kawaida  ya  mwanamke,  pamoja  na  kila  hitaji  ambalo  kama  mwanamke  alitakiwa  kulipata.

Ifahamike  kuwa  habari  ya kutelekeza  inawahusu  wote  mke  na  mme  kwa  maana  ya kuwa  mme  anaweza  kumtelekeza  mke  halikadhalika  mke  anaweza  kumtelekeza  mme. Hata  hivyo  makala  yatazungumzia   mme  kumtelekeza  mke  ambapo sura  ya  29 ,  Sheria ya  ndoa  iliyofanyiwa  marekebisho  mwaka  2010  itarejewa.

1.AINA  ZA  KUTELEKEZA.    

( a ) Aina  ya  kwanza ni  kutelekeza  ambako  mume  anaondoka  kabisa  ndani  ya  nyumba  ambayo  alikuwa  akiishi  na  mke  wake kama  wanandoa  na  kwenda  kuishi  kwingine. Haijalishi huko  alikoenda   panajulikana  ni  wapi au  hapajulikani  suala  la  msingi  ni  kwamba  hayupo  katika  makazi  yake  ya  kawaida  ya familia.

Aidha  ikiwa  hayupo  nyumbani  lakini  kwa  sababu  za  msingi  na za  kisheria  huko  sio  kutelekeza.  Sababu  hizo  ni kama  kuwa  jela, kuwa  hospitali, kuwa  amehamishiwa  sehemu  nyingine kwasababu  ya  matibabu   kwa  mfano  wengine  huamishiwa  mikoani, na pia  kuwa  vitani  labda  baadae  mkapoteza  mawasiliano  na  mazingira  mengine  ya  dharula  za  kibinadamu  na  ambayo  siyo  ya  makusudi   hayawezi  kuitwa  kutelekeza.

( b ) Aina  nyngine  ya kutelekeza  ni   hatua  ya  kuwa  mme  na  mke  wanaishi  wote  katika  nyumba   moja  au  chini  ya paa  moja lakini  mume  huyo  hajishughulishi  na  kutoa  matumizi  au  matunzo  kwa  mke  huyo  kwa  namna  yoyote  ile. Hajui  anakula  nini,  hajui  anavaa  nini, hajui  anapata  vipi  matibabu,  kwa ufupi  hajui  lolote  zaidi  ya  kumuona  tu  kama  binadamu  wengine  ambao  anawaona  mitaani  na  hana  uhusiano  nao.

Pia kuishi  chini  ya  paa  moja  lakini  vyumba  tofauti  nako  ni kutelekeza    hata  kama   mke  anapewa  matumizi  yote  yanayostahili. Zaidi,  hata  kulala  chumba  kimoja  lakini  vitanda  tofauti  kwa  muda  mrefu  tena  kwa  makusudi  kwasababu  ya  mgogoro  wowote  nako  ni kutelekeza.  Lakini  pia  kulala  kitanda  kimoja  bila  kushiriki  tendo  la  ndoa kwa  makusudi  kwa muda mrefu   bila  sababu  za  msingi  za  kiafya au  vinginevyo nako  ni  kutelekeza.

2. NINI  AFANYE  ALIYETELEKEZWA.

Kifungu  cha 115( 1 )( b ) cha  sheria  ya  ndoa  kinasema  kuwa mahakama  inayo  mamlaka  ya  kumuagiza  au  kumuamrisha  mwanaume  kutoa  matunzo  au  matumizi   kwa  mke  wake.  Kwahiyo  kumbe   huna  haja  ya  kulalama  na  kulia  na  hali  tayari  sheria  inaweza  kukusaidia  katika  hili.

Unachotakiwa  kufanya  ni  kwenda  mahakamani   na  kufungua  malalamiko  ambapo  mme  huyo  ataitwa  na  atatakiwa  kujibu  kwanini  hatoi  matunzo   na  hapo  baada  ya  taratibu  za  kimahakama  maamuzi  yatatolewa.  

Kifungu  cha  76  cha  sheria  ya ndoa  kinazitaja  mahakama  ambazo  unaweza  kutumia  katika  kufungua  malalamiko.  Ipo  mahakama  ya mwanzo, ya  wilaya  , ya  hakimu   mkazi na  mahakama  kuu.

Hata   hivyo  unashauriwa  kuanzia  ustawi  wa  jamii ambako  taratibu  zake  ni  nyepesi  na za  muda  mfupi. Ustawi wa  jamii  upo  kila  makao  makuu  ya  wilaya,   ukifika  utauliza  na  utaoneshwa.

Ikishindikana  hapo  sasa  unaweza  kwenda  mahakamani  lakini  pia  unashauriwa  kutumia  mahakama  ya  mwanzo  iliyo  katika  eneo  lako  au  ya  wilaya  iliyo  katika  wilaya   yako . Kwa  kufanya  hivi  hakuna  shaka  habari  ya  kutelekezwa  na  kunyimwa  matumizi  itakuwa  imepatiwa  dawa  sahihi.
MWANDISHI   WA   MAKALA  HAYA   NI   MWANASHERIA  NA  MSHAURI   WA  SHERIA  KUPITIA  GAZETI   LA  JAMHURI   KILA   JUMANNE.  0784482959,  0714047241bashiryakub@ymail.com

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

ALLY KAMWE AZIMIA KWA MKAPA.

RAIS SAMIA KUZINDUA MKUTANO MKUU WA 79 WA BARAZA LA MICHEZO YA MAJESHI DUNIANI

MIGINGO KISIWA KIDOGO ZAIDI AFRIKA KILICHOGOMBEWA NA UGANDA, KENYA