Ujumbe wa Hussein Bashe kwa Waziri Nape baada ya ripoti kumuhusu Makonda


March 22, 2017 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye alikabidhiwa ripoti na Kamati aliyoiunda kwa ajili ya kuchunguza tukio la tuhuma za uvamizi alioufanya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda katika ofisi za Clouds Media Group usiku akiwa na askari wenye silaha.
Waziri Nape baada ya kupokea ripoti hiyo aliongea na Waandishi wa Habari kueleza kuwa hatua inayofuata ni yeye kuiwasilisha ripoti hiyo katika ngazi kuu ya uongozi akiwemo Rais Magufuli ili hatua stahiki iweze kuchukuliwa.
Baadhi ya walioonesha kuipokea taarifa za ripoti hiyo ni pamoja na Mbunge wa Nzega mjini Hussein Bashe ambaye akaamua kuandika ujumbe kupitia account yake ya Twitter huku akipongeza hatua ya Waziri Nape.
Bashe ameandika…>>>’Hongera sana Comrade Nape na kamati yako, Umewatendea haki watanzania na Umetimiza wajibu wako.” ‘Voice of Justice ‘
Comrade Nape umelinda heshima ya tasnia ya habari, chama chetu na nchi yetu.‘ – Hussein Bashe

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.