WAJUMBE WA KAMATI YA BUNGE YA HESABU ZA SERIKALI WATEMBELEA MIRADI YA NHC JIJINI DAR ES SALAAM


Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC Bw. Nehemia Mchechu akitoa taarifa ya shirika hilo kwa kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali wakati kamati hiyo ilipotembelea miradi ya shirika hilo iliyopo jijini Dar es salaam, Kamati hiyo imesifu kazi zinazofanywa na shirika hilo kutokana na kuendeleza miradi mbalimbali ya ujenzi wa majengo ya kuuza na kupangisha.
Mh. Haji Mponda Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali akizungumza na Mama Blandina Nyoni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC
Mkurugenzi wa Ubunifu shirika la nyumba la NHC Bw. Issack Peter akitoa maelezo kwa wajumbe wa kamati ya bunge ya Hesabu za serikali wakati waliptembelea miradi ya shirika hilo inayojengwa jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba NHC Bw. Nehemia Mchechu akizungumza na waandishi wa habari wakati Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali ilipotembelea miradi ya shirika hilo.
Wajumbe wa Kamti ya Bunge ya Hesabu za Serikali wakitembelea mradi wa 711 unaotekelezwa na shirika hilo uliopo Kawe
Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba NHC Bw. Nehemia Mchechu akitoa maelezo kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali ilipotembelea kwenye miradi hiyo.
Mkurugenzi wa Fedha NHC Bw. Felix Maagi akizungumza na mmoja wa wajumbe wa kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali waliotembelea katika miradi ya NHC.
Wajumbe wa Kamti hiyo Munde Tabwe kushoto na mama Burra wakijadiliana jambo wakati kamati hiyo ilipotembelea katika miradi ya shirika hilo jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba Mama Blandina Nyoni akizungumza na Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba NHC Bw. Nehemia Mchechu na mkurugenzi wa Ubunifu Isaack Peter.
Isaack Peter Mkurugenzi wa Ubunifu NHC akitoa maelezo kwa wajumbe wa kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali wakati walipotembelea miradi ya shirika hilo jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Kamti ya Bunge ya Hesabu za serikali Mh. Haji Mponda akiuliza swali kwa Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba NHC Bw. Nehemia Mchechu wakati wajumbe wa kamati hiyo walipotembelea katika miradi ya shirika hilo jana.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.