Wanaodaiwa na Bodi ya Mikopo watakiwa kulipa madeni yao


Benjamin Sawe
Maelezo.
Bodi ya mikopo ya Elimu ya Juu nchini imewataka wanaodaiwa na Bodi hiyo kurejesha mikopo yao ili na wengine waweze kukopa badala ya kusubiri kuchukuliwa hatua.
Akiongea katika kipindi cha Tunatekeleza kinachorushwa na Televisheni ya Taifa (TBC) Mkurugenzi wa Bodi ya mikopo ya Elimu ya Juu Abdul Badru alisema tangu waanze mfumo wa kuwabana wadaiwa kupitia waajiri wao kasi ya urejeshwaji mikopo imeongezeka.
Alisema pamoja na kuwabana pia wamekuwa wakitoa elimu kuhusu umuhimu wa kurejesha mikopo hiyo pamoja na kutunga sheria ya kuwabana wasiolipa mikopo.

Awali kabla ya kuwekwa kwa msukumo katika kudai mikopo hiyo urejeshwaji ulikuwa wastani wa shilingi bilioni 5 mpaka 6 kwa mwezi lakini kwa sasa wanapata marejesho ya mikopo zaidi ya Bilioni 10.Bw. Badru alisema hivi sasa wameboresha mfumo wa utoaji mikopo kwa kuziba mianya ya wanafunzi hewa pamoja na wale wasiokuwa na sifa ambao wamekuwa wakipeleka vielelezo vya uongo.
Alisema licha ya kupitishwa kwa orodha ya wanafunzi wanaostahili mikopo uhakiki umekuwa ukifanyika kila baada ya miezi mitatu ambapo maofisa wa bodi hiyo huenda vyuoni ili kujiridhisha kama wanafunzi waliolengwa kwenye mikopo hiyo wapo.
“Kwa mfano mwaka jana wanafunzi elfu tatu miongoni mwa walioomba mikopo kwa madai ya kufiwa na wazazi waliwasilisha vyeti vya Vifo vya wazazi wao ambavyo baada ya kupelekwa RITA walishindwa kuvitambua”Alisema BADRU.
Alisema mwanafunzi anayekosa mkopo kama anavyo vigezo vyote vinavyotakiwa hutakiwa kukata rufaa ili ufanyike upitiaji upya wa nyaraka zake.
Kwa mwaka wa fedha 2016/2017 jumla ya shilingi Bilioni 483 zimetengwa kwaajili ya kuwakopesha wanafunzi 120,000 kutoka vyuo tofauti nchini.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.