KATIBU MKUU WIZARA YA HABARI AHUDHURIA SEMINA YA MAENDELEO YA REDIO,TELEVISHENI KIDIJITALI CHINA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Elisante Ole Gabriel, akitoa hutuba hivi karibuni wakati wa ufunguzi wa semina ya saba kujadili jinsi ya ushirikiano na maendeleo ya televesheni ya kidigitali barani Afrika iliyofanyika Mjini Beijing nchini China.

 Abraham Ntambara

WAJUMBE zaidi ya 400 kutoka nchi 46 za Afrika na Asia wameshiriki semina iliyofanyika juzi Mjini Beiging China, kujadili jinsi ya kufanikisha ushuirikiano katika maendeleo kwenye sekta ya  redio na televisheni za kidigitali.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na Ofisa Uhusiano wa StarTimes Josephine Stephen ilisema  semina hiyo ni ya saba kufanyika na walianza kuendesha semina hizo tangu mwaka 2011.

Alitaja baadhi ya nchi zilizoshiriki ni Nigeria, Jamuhuri ya Afrika ya Kati, Chad, Guinea, Liberia, Malawi, Zambia, DRC Congo na Ethiopia ambapo pia ulihudhuriwa  na mawaziri wanaohusika na masuala ya mawasiliano zaidi ya 30 nchi hizo za Afrika.

Akitoa hotuba wakati wa ufunguzi Rais wa Startimes Group, Pang Xinxing alisema kuwa semina hizo zimekuwa zikisaidia katika kuongeza ushirikiano na mazungumzo ya pamoja  kwa ajili ya maendeleo ya sekta ya redio na TV katika Afrika.

“Startimes iko tayari kukamilisha kuweka setilaiti katika vijiji elifu 10 Elfu chini ya mradi  na maelekezo ya serikali ya Kichina na Afrika. Mradi huu unaitwa China-Africa ni  ushirikiano ulitangazwa na Rais wa China Xi Jinping wakati wa mkutano maalumu na nchi za Afrika uliofanyika 2015 Johannesburg nchini Afrika Kusini,” alisema Xinxing.

Naibu Waziri wa China anayeshughulikia masuala ya Utawala wa Habari za Uchapishaji, Redio, Filamu na Televisheni Tong Gang, alisema ushirikiano kati ya vyombo vya habari vya China na Afrika unaunganishwa na chama cha utetezi cha Kichina kinachojulikana kama  ‘mkanda mmoja na njia moja’.

Aidha alisema China iko tayari kushirikiana zaidi katika nyanja hii ya maendeleo kwa vyombo vya habari katika kuhamia kidigitali nchini Afrika.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Tanzania  Elisante Ole Gabriel, alibainisha kuwa semina ilitoa fursa kwa nchi za Afrika kushiriki uzoefu wao kuhusu upanuzi wa teknolojia ya digital na pia mipango ya baadaye.

Alisema kuwa Startimes ilikuwa imetoa jukwaa kwa ajili ya Tanzania kupanua upatikanaji wa televisheni za kidigitali  ili kufikia mafanikio ya nchi kwa kuongeza vyanzo vingine vya  kiuchumi.
mwisho

0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

NAMAINGO YAZINDUA HEKA 7000 ZA MASHAMBA MJI KIJIJI CHA MSOLWA, MKURANGA

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

DIAMOND AITWA NA NYOTA YAJAA GOMS

HABARI MPASUKOOO:GARI LAGONGA WATOTO KUIKWEPA BODABODA GONGO LA MBOTO

HARAMBEE YA UJENZI HOSPITALI YA MUHEZA YAVUKA MALENGO, ZAPATIKA BIL. 1.6

WAZIRI SHONZA AMJIBU DIAMOND

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

HABARI MPASUKOOO!!! MCHAWI ADONDOKA AKIWA UCHI KIVULE,DAR