MASHINDANO YA DASANI MARATHON KUFANYIKA MEI 14 DAR

 Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Coca Cola, Nakala Hettiarachch (Kulia ) akiwaeleza wanahabari jijini Dar es Salaam leo, kuhusu mashindano ya Dasani Marathon yanayotarajia kuanza Mei 14, mwaka huu jijini Dar es Salaam na Mgeni rasmi atakuwa Mwanariadha mstaafu wa Kimataifa, Juma Ikangaa. Kushoto ni Rais wa Dar running club , Goodluck Elvis. (PICHA NA DALILA SHARIF).

Abraham Ntamabara
MWANARIADHA wa Mstaafu wa Kimataifa Juma Ikangaa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mashindano ya riadha ya Dasani Marathon yatakayo fanyika mei 14 mwaka huu jijini Dar es salaam.
Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Coca-cola Nalaka Hetterachchi wakati akizungumza na vyombo vya habari, alisema dhamira ya mashindano hayo ni kuendeleza mchezo Wa riadha pamoja na kukuza uchumi  nchini.
“Coca-cola imedhamini mbio hizi, washiriki watakimbia katika mbio za kilomita 10 na 21, zitashirikisha wakimbiaji zaidi ya 1000 ambapo zawadi mbali mbali zitatolewa kwa washindi, mshindi wa kwanza atajinyakulia medali,” alisema Hetterachchi.
Mwanariadha Mstaafu Juma Ikangaa alisema ili mshiriki aweze kupata ushindi katika mashindano hayo ni lazima ujiandae, hivyo amewaomba wadau mbali mbali wajitokeze ili kuweza kushinda medali hizo.
Juma alisema kuwa, angefurahi  kuona rekodi ya kimataifa ya watu maarufu katika mbio hizo ili kuleta mabadiliko  katika tasnia ya michezo ulimwenguni kote pamoja na kutoa hamasa kwa Vijana.
Kwa upande wa Rais wa  Dar Running club Goodluck Elvis alibainisha kuwa mbio hizo zilianza miaka mitatu iliyopita na zimekuwa zikipata umaarufu. Alieleza kwamba wamejiandaa vya kutosha ili kuhakikisha usalama unakuwepo siku ya mashindano.
Aliwataka wananchi kujitokeza kuchukua fomu za kujisajili ili kushiriki katika mashindano hayo. Alitaja vituo vya kuchukulia fomu hizo kuwa ni Colosseum Gym masaki, shoppers supermarket mikocheni na mlimani city Mall.
Mwisho


0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

LICHA YA UZURI WAKE MWANADADA ELIZABETH MICHAEL a.k.a LULU SI MALI KITU MBELE YA RAY, AMKWEPA KUOGOPA AIBU.

IJUE HISTORIA YA UHASIMU WA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA

PICHA:NYOKA AINA YA CHATU AUWAWA KANISANI BAADA YA KUKUTWA NYUMBANI KWA MFANYABIASHARA MAARUFU JIJINI ARUSHA AKISADIKIWA KWA IMANI ZA KISHIRIKINA

WENGI WAJITOKEZA KUMUAGA MPENDWA WAO MWANAHABARI JOYCE MMASI