4x4

PLUIJM NA SINGIDA UNITED YAKE HAO MDOGOMDOGO NDANI YA MWANZATimu ya soka ya Singida United ya mkoani Singida ambayo imepanda daraja hivi karibuni na itashiriki michuano ya Ligi Kuu Bara msimu ujao, ipo mbioni kuhamishia makazi yake kwa muda jijini Mwanza.

Hatua hiyo imekuja baada ya kocha mkuu wa timu hiyo, raia wa Uholanzi,  Hans van Der Pluijm kuutaka uongozi wa klabu hiyo kufanya hivyo kutokana na hivi sasa kutokuwa na uwanja wa kufanyia mazoezi baada ya ule wa Namfua ambao ndio inaoutumia kuwa kwenye matengenezo.

Mwenyekiti wa Singida United, Yusuph Mwandami, amesema kuwa baada ya mapendekezo hayo ya Pliujm, kwa pamoja walikubaliana na ushauri huo, hivyo muda wowote mambo yatakapokuwa sawa, timu hiyo itaenda kukaa kwa muda jijini Mwanza.

“Hata hivyo, pindi uwanja wetu wa Namfua utakapokuwa tayari, basi timu itarudi Singida kuendelea na maandalizi yake kwa ajili ya ligi kuu.

“Niwaombe tu wapenzi na mashabiki wetu, hususan wakazi wa mkoani Singida, kuwa wavumilivu katika kipindi chote ambacho timu yao itakapokuwa Mwanza,” alisema Mwandami.
Post a Comment