RAIS MAGUFULI AKIPOKEA RIPOTI YA TUME YA UCHUNGUZI YA MCHANGA WA MADINI

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza wakati wa hafla ya kupokea ripoti ya kamati ya kwanza ya iliyoiunda kwa ajili ya kuchunguza kiwango cha madini kilichopo kwenye mchanga wa madini (Makinikia) uliokamatwa katika bandari ya Dar es Salaam ukiwa katika makontena 277 tayari kwa kusafirishwa nje ya nchi. Kutoka kulia ni Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Mhandisi John Kijazi. 
 : Mwenyekiti wa Kamati ya kwanza ya Wataalam wa Jiolojia iliyoiundwa kwa ajili ya kuchunguza kiwango na aina ya madini  yaliyopo kwenye mchanga wa madini (Makinikia), Profesa Abdulkarim Hamis Mruma akiwasilisha ripoti yao mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli (hayupo pichani) wakati hafla ya kuwasilisha ripoti hiyo Ikulu jijini Dar es Salaam leo. Kamati hiyo ya watu wanane iliundwa kufuatia kukamatwa kwa makontena 277 yakiwa na mchanga huo katika bandari ya Dar es Salaam tayari kwa kusafirishwa nje ya nchi. Kutoka kulia ni Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Mhandisi John Kijazi. 
 : Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea ripoti kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya kwanza ya Wataalam wa Jiolojia iliyoiundwa kwa ajili ya kuchunguza kiwango na aina ya madini  yaliyopo kwenye mchanga wa madini (Makinikia), Profesa Abdulmalik Mruma katika hafla iliyofanyika leo Ikulu Jijini Dar es Salaam. Kamati hiyo iliundwa kufuatia kukamatwa kwa makontena 277 yakiwa na mchanga huo katika bandari ya Dar es Salaam tayari kwa kusafirishwa nje ya nchi. Kutoka kulia ni Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipitia ripoti ya Kamati ya kwanza ya Wataalam wa Jiolojia iliyoiundwa kwa ajili ya kuchunguza kiwango na aina ya madini  yaliyopo kwenye mchanga wa madini (Makinikia)

 Wajumbe wa Kamati ya Kwanza ya Wataalam wa Jiolojia iliyoiundwa kwa ajili ya kuchunguza kiwango na aina ya madini yaliyopo kwenye mchanga wa madini (Makinikia) wakiwa tayari kwa kuwasilisha ripoti yao katika hafla iliyofanyika Ikulu leo Jijini Dar es Salaam. Kamati hiyo iliundwa tarehe 29 Machi 2017, kufuatia kukamatwa kwa makontena 277 yakiwa na mchanga huo katika bandari ya Dar es Salaam tayari kwa kusafirishwa nje ya nchi. Wajumbe wa Kamati hiyo iliyoongozwa na Mwenyekiti wake Profesa Abdulkarim Hamis Mruma, wengine ni Profesa Justianian Rwezaura Ikingula, Profesa Joseph Bushweshaiga, Dk Yusuf Ngenya, Dk Joseph Yoweza Philip, Dk Ambrose Itika, Mohamed Zengo Makongoro na Hery Issa Gombela.

 Mkuu wa Jeshi la Ulinzi Tanzania – JWTZ, (CDF) Venance Mabeyo akiteta jambo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji George Masaju alipokutana nao katika hafla ya kukabidhi ripoti ya Kamati ya kwanza ya Wataalam wa Jiolojia iliyoiundwa kwa ajili ya kuchunguza kiwango na aina ya madini  yaliyopo kwenye mchanga wa madini (Makinikia) Ikulu Jijini Dar es Salam leo.
 Wasanii wa Kundi la Tanzania All Stars wakitumbuiza wimbo wa kuhamasisha uzalendo wakati wa hafla ya kukabidhi ripoti ya Kamati ya kwanza ya Wataalam wa Jiolojia iliyoiundwa kwa ajili ya kuchunguza kiwango na aina ya madini  yaliyopo kwenye mchanga wa madini (Makinikia) Ikulu Jijini Dar es Salam leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Joseph Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Kamati ya kwanza ya Wataalam wa Jiolojia iliyoiundwa kwa ajili ya kuchunguza kiwango na aina ya madini  yaliyopo kwenye mchanga wa madini (Makinikia) Ikulu Jijini Dar es Salam leo. Kamati hiyo iliundwa tarehe 29 Machi 2017, kufuatia kukamatwa kwa makontena 277 yakiwa na mchanga huo katika bandari ya Dar es Salaam tayari kwa kusafirishwa nje ya nchi.

Picha na: Frank Shija - MAELEZO

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.